Wednesday, 25 February 2015

Mhe. Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto), Katibu Mkuu Bi. Joyce Mapunjo (kulia) wakiwa katika Mkutano na Waandishi wa habari (hawapo pichani) uliofanyika Wizarani 22/02/2015
Waziri Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (watatu kushoto kati ya walioketi) kushoto kwake ni Katibu Mkuu Bi. Joyce Mapunjo wakiangalia namna Mfumo wa kufanya Mikutano kwa njia ya Video unavyofanya kazi wengine katika picha ni Watumishi wa Wizara na Waandishi wa Habari.
Mhe. Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Mkutano na wandishi hao uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, uliopo jengo la Water Front Dar-es-Salaam 22/02/2015

Mhe. Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe akisisitiza jambo wakati akihojiwa na waandishi wa habari mara baada ya Mkutano na waandishi hao 22/02/2015.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wapili kushoto) wengine (kushoto kwake) ni Mkurugenzi Idara ya Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu Bi. Mary Fidelis, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Mipango Bi. Graceana Shirima, Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi Bi. Asina Kisinzah na  Mkurugenzi Msaidizi  Idara ya Miundombinu ya Kiuchumi na Huduma za Kijamii Bw. Eliabi K. Chodata wakipata maelezo kutoka kwa Mtaalam  Bw. Salum Mohamed Nalolah kuhusu Mfumo wakufanya Mikutano kwa Njia Video unavyofanya Kazi.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (katikati), Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu Bi. Mary Fidelis (kulia) wakipata maelezo kutoka kwa Mtaalam Bw. Salum Mohamed kuhusu namna ya mfumo wa kufanya  Mikutano kwa Njia ya Video unavyofanya kazi.


Waziri Wizara ya Sayansi na Teknologia Mhe. Prof. Makame Mbalawa (kulia) akiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kushoto) siku ya uzinduzi wa Mfumo wa kufanya mikutano kwa njia ya Video

Waziri wa Wizara ya Sayansi na Teknologia Mhe. Prof. Makame Mbarawa 
(kulia)Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (katikati), na Mkurugenzi wa
 Idara ya Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu Bi. Mary Fidelis wakiwa katika uzinduzi wa mfumo wa kufanya Mikutano kwa njia ya Video.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akisaini kitabu cha wageni alipohudhuria uzinduzi wa Mfumo wa  kufanya Mikutano kwa Njia ya Video, uliofanyika Wizarani Dar-es-Salaam Februari 20, 2015.

Wednesday, 18 February 2015

MKUTANO WA 16 WA VIONGOZI WAKUU WA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUFANYIKA NAIROBI, KENYA.JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MKUTANO WA 16 WA VIONGOZI WAKUU WA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUFANYIKA NAIROBI, KENYA
Mkutano wa 16 wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki unatarajiwa Kufanyika 20 Februari, 2015 Nairobi, Kenya katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta. Mkutano huu utatanguliwa na Mkutano wa dharura wa  Baraza la Mawaziri la Jumuiya Jumuiya Afrika Mashariki. Pamoja na mambo mengine Mkutano wa Viongozi wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya  Afrika Mashariki unatarajia kufanya yafuatayo;
·         Kupitia taarifa ya Mwaka ya Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kipindi cha Disemba 2013 hadi Novemba 2014,
·         Kupitia taarifa ya utekelezaji wa maamuzi ya Vikao vya Jumuiya ya Afrika     Mashariki
·         Kupitia taarifa ya Masuala ya kiutumishi yakiwemo; uteuzi wa Jaji wa Mahakama ya Rufaa ya Jumuiya Afrika Mashariki, Jaji wa Mahakama ya kwanza ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, uteuzi wa Naibu katibu Mkuu wa Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Jamhuri ya Burundi na kuongeza Muda wa Mkataba wa Naibu katibu Mkuu wa Jumuiya kutoka Jamhuri ya Uganda.
Aidha katika Mkutano huu wa Wakuu wa Nchi wanatarajia kuzindua mpango wa kisasa wa kufanya Mikutano kwa Njia ya Video. (Video Confrence)

Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaotararijiwa kuhudhuria katika Mkutano huu ni Mhe. Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania, Mhe. Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi, Mhe. Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda, Mhe. Rais Paul Kagame wa Rwanda, na  Mhe. Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ambaye ni mwenyeji wa Mkutano.

Imetolewa na;
Katibu Mkuu
WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI


Tuesday, 17 February 2015

(Mstari wa mbele Kushoto - Kulia) Ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji Dkt. Abdulla Makame, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Miundombinu ya Kiuchumi na Huduma za Kijamii Eng. Abdillah Mataka, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Zanzibar Bw. Salum Maulid Salum, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama Bw. Amani P. Mwatonoka wakiwa katika Picha ya Pamoja na Waandishi Wahabari kutoka Unguja na Pemba, Mjini Unguja 11 Februari, 2015.


Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Miundombinu ya Kiuchumi na Huduma za Kijamii Eng. Abdillah Mataka akiwasilisha Mada kwenye Warsha iliyoandaliwa na Wizara kwa Waandishi wa Habari wa Unguja na Pemba (hawapo pichani), Februari 2015.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama Bw. Amani P. Mwatonoka akiwasilisha Mada kwenye Warsha iliyoandaliwa na Wizara kwa Waandishi wa Habari wa Unguja na Pemba (hawapo pichani), Februari 2015.

Mtaalam wa Mawasiliano wa Wizara Bw. Faraja Mgwabati akiwasilisha Mada  kwenye Warsha iliyoandaliwa na Wizara kwa Waandishi wa Habari wa Visiwa  vya Unguja na Pemba iliyofanyika Mjini Unguja 11 Februari, 2015.

Katibu Mkuu Bi. Joyce Mapunjo (mbele katikati), Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar Bw. Said A.S Natepe (wakwanza kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa ZBC na Maafisa wa Wizara mbele ya Jengo la Kamisheni ya Kiswahili.

Katibu Mkuu wa Wizara Bi. Joyce Mapunjo akisaini kitabu cha Wageni kwenye Ofisi ya Wizara iliyopo Zanzibar alipotembelea Ofisi hiyo, Kulia ni Afisa wa Wizara Bw. Othuman Maalim Othuman Februari, 2015.