Thursday 13 August 2015

MKUTANO WA 32 WA BARAZA LA MAWAZIRI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
Simu ya maandishi: ‘MEAC’
Simu Na. 022-2126827, 2126830, 2126823
Fax: 022 – 2126651/2120488
Barua Pepe: ps@meac.go.tz
  •  

NSSF Waterfront Ghorofa ya 5
35 Barabara ya Edward Sokoine S.L.P. 9280,              
11467 DAR ES SALAAM.                
13/08/ 2015.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MKUTANO WA 32 WA BARAZA LA MAWAZIRI
Mkutano wa 32 wa Baraza la Mawaziri unatarajiwa kufanyika kesho tarehe 14 Agosti,2015 Jijini Arusha Tanzania. Mkutano huu wa Baraza la Mawaziri unafanyika kesho ukiwa umetanguliwa na Vikao vya Maafisa Wandamizi wa Serikali na Kamati ya Uratibu (Makatibu Wakuu) ambavyo vilifanyika kuanzia tarehe10 hadi 13 Agosti, 2015.
Pamoja na mambo mengine Baraza la Mawaziri litajadili na kuzingatia mambo yafuayo;
  • Taarifa ya Tume ya Ukaguz
  • Taarifa ya utekelezajia wa mazimio yalifanywa na Mkutano wa Baraza la Mawaziri uliopita
  • Taarifa ya Mkutano wa 22 wa Kisekta wa Baraza la Mawaziri wanaosimamia masuala na mipango ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
  • Taarifa ya Kikosi kazi cha ngazi ya juu kinacho shughulikia masuala ya marekebisho ya Mkataba wa uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Vilevile moja ya ajenda itakayo jadiliwa katika Mkutano huu wa 32 wa Baraza la Mawaziri itahusu Mkutano wa kwanza wa Kilele wa Wafanyabiashara wanaomiliki Viwanda vya Uzalishaji uanaotarajiwa  kufanyika Jijini Kampala, Uganda tarehe 1 hadi 2, Septemba 2015.

Aidha, Baraza litajadili na kuzingatia ripoti kutoka taasisi mbalimbali zilizopo chini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwemo ripoti ya Taasisi ya Shirikisho la Vyuo Vikuu vya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki

Imetolewa na;
Katibu Mkuu
WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI




Monday 10 August 2015

HABARI KATIKA PICHA ZA MATUKIO YALIYOJILI KWENYE MAONESHO YA KITAIFA YA NANENANE

Taswira ya Banda la Wizara lililotumika kutoa elimu kwa umma kwenye maonesho ya Nanenane.Maonesho hayo mwaka huu Kitaifa yamefanyika Mkoani Lindi kuanzia tarehe 1-8/08/2015
Taswira ya Banda la Wizara lililotumika kutoa elimu kwa umma kwenye maonesho ya Nanenane.Maonesho hayo mwaka huu Kitaifa yamefanyika Mkoani Lindi kuanzia tarehe 1-8/08/2015
Watumishi wa Wizara wakiwa kwenye banda la Wizara siku ya ufunguzi wa maonesho ya Nanenane tayari kwa kutoa elimu kwa umma Mkoani Lindi Tarehe 01/08/2015.
Naibu Katibu Mkuu Bw. Amantius Msole akizungumza na mmoja wa Maafisa wa Wizara alipotembelea banda lililotumika kutoa elimu kwa umma kwenye Maonesho ya Kilimo maarufu Nanenane yaliyofanyika Mkoani Lindi 01/08/2015.
Naibu Katibu Mkuu Bw. Amantius Msole akizungumza na Maafisa wa Wizara alipotembelea banda lililotumika kutoa elimu kwa umma kwenye Maonesho ya Kilimo maarufu Nanenane 01/08/2015.
Naibu Katibu Mkuu Bw. Amantius Msole (katikati aliyevalia tai) akiwa kwenye sherehe ya ufunguzi wa Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Lindi 01/08/2015.