Friday 30 October 2015

MKUTANO WA MAANDALIZI YA MAONESHO YA JUAKALI/NGUVUKAZI

Wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya Maonesho ya Juakali/Nguvukazi wakiwa katika mkutano wa maandalizi kwa njia ya Video 'Video conference' katika ukumbi wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki. kutoka kulia ni Bi. Vivian Rutaihwa- Afisa Biashara(MEAC), anayefuata ni Bw. Josephat Rweymamu Mwenyekiti wa CISO, Bw. Joseph Nganga- Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Kazi na Ajira, Bw. Ally M. Ahmed-Mkurugenzi Idara ya Kazi na Ajira na Mwisho ni Bw. Juvenal Lema - Mchumi Mwandamizi (MEAC)

Tuesday 27 October 2015

HAFLA YA KUWAPONGEZA NA KUWAKABIDHI VYETI WAFANYAKAZI BORA 22/10/2015

Katibu Mkuu Bibi Joyce Mapunjo (aliyesimama) akifuarahia jambo na wafanyakazi wa Wizara kwenye hafla ya kuwatunuku vyeti wafanyakazi bora iliyofanyika katika ukumbi mdogo wa mikutano wa Wizara uliopo katika Jengo la WaterFront Dar es Salaam 22/10/2015
   Katibu Mkuu Bibi Joyce Mapunjo (aliyesimama) akifuarahia jambo na wafanyakazi wa Wizara kwenye hafla ya kuwatunuku vyeti wafanyakazi bora iliyofanyika katika ukumbi mdogo wa mikutano wa Wizara uliopo katika Jengo la WaterFront Dar es Salaam 22/10/2015
Katibu Mkuu Bibi Joyce Mapunjo (kulia) akizungumza na watumishi wa baada ya kuwatunuku vyeti wafanyakazi bora
Naibu Katibu Mkuu Bw. Amantius Msole (kushoto aliyesimama) akizungumza na wafanyakazi (hawapo pichani) kwenye hafla ya kuwapongeza wafanyakazi bora iliyofanyika katika ukumbi mdogo wa mikutano wa Wizara katika Jengo la WaterFront Dar es Salaam 22/10/2015
Katibu Mkuu Bibi Joyce Mapunjo (kulia) akimpongeza Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bibi Robi Bwiru (kushoto) baada ya kumtunuku cheti cha mfanyakazi bora. Tukio hili lilifanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, uliopo katika jingo la WaterFront Dar-es-Salaam 22/10/2015
Katibu Mkuu Bibi Joyce Mapunjo (kulia) akimpongeaza Mkurugenzi Msaidizi wa Sera na Mipango Bw. Oswald Kyamani baada ya kumtunuku cheti cha mfanyakazi bora. Tukio hili lilifanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, uliopo katika jengo la WaterFront Dar-es-Salaam 22/10/2015
Katibu Mkuu Bibi Joyce Mapunjo (kulia) akimpongeaza Mkurugenzi Msaidizi Rasilimali Watu Bw. Hamid Mbegu (kushoto) baada ya kumtunuku cheti cha mfanyakazi bora. Tukio hili lilifanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, uliopo katika jengo la WaterFront Dar-es-Salaam 22/10/2015
Katibu Mkuu Bibi Joyce Mapunjo (kulia) akimtunuku cheti cha mfanyakazi bora Mhasibu Bibi Neema Lemunge (kushoto) . Tukio hili lilifanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, uliopo jingo la WaterFront Dar-es-Salaa
    Katibu Mkuu Bibi Joyce Mapunjo (kulia) akimtunuku cheti cha mfanyakazi bora Afisa Rasilimaliwatu Mkuu Bibi Ester Masigo (kushoto) 22/10/2015
Katibu Mkuu Bibi Joyce Mapunjo (kulia) akimtunuku cheti cha mfanyakazi bora Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bw. Petro Lyatuu (kushoto).Tukio hili lilifanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, uliopo jengo laWaterFront Dar-es-Salaam 22/10/2015
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi Rasilimaliwatu Bibi Mary Fidelis (aliyesimama kulia) akimkaribisha Katibu Mkuu kwenye hafla ya kuwapongeza na kuwatunuku vyeti wafanyakazi bora. Tukio hili lilifanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, uliopo katika jengo la WaterFront Dar-es-Salaam 22/10/2015.
Katibu Mkuu Bibi Joyce Mapunjo akizungumza na wafanyakazi kabla ya kuanza kuwapongeza na kuwatunuku vyeti wafanyakazi bora. Tukio hili lilifanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, uliopo katika jingo laWaterFront Dar-es-Salaam 22/10/2015.
Katibu Mkuu Bibi Joyce Mapunjo akimtunuku Bibi Asha Kisumo cheti cha mfanyakazi bora 22/10/2015 





Wednesday 21 October 2015

HABARI KUHUSU TIMU YA WAANGALIZI WA UCHAGUZI OCTOBA 25, 2015 YA EAC

     Katibu Mkuu Bibi Joyce Mapunjo (wa kwanza kushoto kati ya waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na timu ya waangalizia wa uchaguzi Nchini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki mara baada ya mkutano na wanahabari uliofanyika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar 20/10/2015.
      Kiongozi wa timu ya uangalizi wa uchaguzi nchini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambaye pia ni Makamu wa Rais wa zamani wa Kenya Mhe. Dkt. A. A Moody Awori akiongea kwenye mkutano na wanahabari uliofanyika katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar 20/10/2015
     Katibu Mkuu Bibi Joyce Mapunjo akiongea kwenye Mkutano na wanahabari (hawako pichani) uliondaliwa na Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar 20/10/2015
    Mmoja wa waangalizi wa Uchaguzi Nchini kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Charles Njoroge akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kwenye mkutano uliofanyika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es Salaam 20/10/2015.  
      Naibu Katibu Mkuu Bw. Amantius C. Msole (kulia), Mkurugenzi Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama Bw. Stephen Mbundi (katikati) na mmoja wa waangalizi wa uchaguzi kutoka SADC (kushoto) wakiwa kwenye Mkutano na wanahabari uliondaliwa na Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es Salaam 20 Oktoba, 2015.
Katibu Mkuu Bibi Joyce Mapunjo (katikati) akiwa kwenye mkutano na wanahabari ulioandaliwa na Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kushoto ni Mbunge wa EALA Mhe. Peter Muthuki, na Makamu wa Rais wa zamani wa Kenya Mhe. Dkt. A. A Moody Awori (kulia) ambaye pia ni Kiongozi wa timu ya waangalizi wa uchaguzi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.




WAANGALIZI WA UCHAGUZI KUTOKA EAC WAHIMIZWA KUZINGATIA SHERIA NA TARATIBU NCHINI.

Kuelekea uchaguzi Mkuu Nchini unaotarajiwa kufanyika tarehe 25 Oktoba, 2015 Jumuiya ya Afrika Mashariki imeleta timu ya waangalizi yenye jumla ya watu 55 inayohusisha wataalamu na viongozi mbalimbali wa kitaifa wakiwemo wastaafu na wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka nchi wanachama. Timu hii iliwasili Jijini Dar es Salaam 18 Oktoba, 2015. 

Katibu Mkuu Bibi Joyce Mapunjo akizungumza kwenye Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jana katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es Salaam ambao pia ulihudhuriwa na waangalizi kutoka EAC na SADC amewahimiza waangalizi wa uchaguzi kuzingatia sheria na taratibu za Nchi katika shughuli zao. 

Akizungumza katika mkutano huo alisisitiza kuwa Tanzania ni Nchi ya Kidemokrasia na inautaratibu mzuri wa kuachiana madaraka ambapo uchaguzi hufanyika kila baada ya miaka mitano na kubadilsha uongozi wa juu kila baada ya miaka kumi kwa mujibu wa katiba. 

Kiongozi wa timu ya Uchunguzi kutoka EAC ambaye pia ni Makamu wa Rais wa zamani wa Kenya Mhe. Dkt. A. A Mood Awori akizungumza katika Mkutano huo aliipongeza Tanzania kwa kudumisha Demokrasia na Utawala wa kisheria na kuongeza kuwa katika uchaguzi huu Tanzania iendeleze utamaduni wa kudumisha Demokrasia, Utawala Bora na uwajibikaji ili iendelee kuwa na amani na utulivu. 

Timu ya waangalizi ya EAC ambayo itafanya kazi katika vipindi vitatu vinavyotajwa kuwa, Kabla ya uchaguzi, wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi itaangalia mambo yafuatayo; 

· Ushirikishwaji wa vyombo vya habari katika kuripoti masuala        mbalimbali ya uchaguzi 

· Muda wa kutosha wa kampeni 

· Uhuru wa kuendesha shughuli za kisiasa pasipo fujo au vitisho 

· Utolewaji wa elimu ya uraia na upigaji kura 

· Upigaji kura kwa siri, na 

· Ubora wa vifaa vya uchaguzi 

Aidha timu hiyo ya waangalizi itafanya kazi yake Tanzania bara na Visiwani wakati wote wa uwepo wake katika kipindi chote cha uchaguzi. 



Wednesday 14 October 2015

WANACHAMA WAPYA WAWILI WAAPISHWA BUNGE LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI.



WANACHAMA WAPYA WAWILI WAAPISHWA BUNGE LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI.

Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (BJAM) katika Mkutano wake wa pili (2), kipindi cha Nne (4) cha Bunge la tatu linaloendelea Jijini Nairobi; tarehe 7 Oktoba , 2015 lilisimamia kiapo cha utii wa Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa wanachama wapya wawili (2) waliojiunga na Bunge hilo.

Bunge lilimwapisha Waziri wa Wizara ya Masuala ya Afrika Mashariki kutoka Jamhuri ya Burundi Mhe. Leontine Nzeyimana ambaye ameteuliwa tena kuiongoza Wizara hiyo.

Mhe. Dkt. Francois Xavier Kalinda, ambaye ni Mbunge mpya toka Nchini Rwanda pia aliapishwa katika Mkutano huo, kiapo kiliongozwa na Katibu wa BJAM Bw. Kenneth Madete mbele ya Spika wa Bunge hilo Mhe. Daniel F. Kidega.Wote wawili waliapa kwa mujibu wa kanuni ya 5 (4) ya Kanuni za Bunge la BJAM inayosema; “Hakuna Mbunge anaweza kukaa au kushiriki katika vikao vya Bunge mpaka hapo kiapo cha kudhihirisha utii kwa Mkataba kitakapo chukuliwa" (No Member can sit or participate in the proceedings of the House until the Oath or Affirmation of Allegiance to the Treaty is taken”)

Kabla ya kuchaguliwa na Bunge la Rwanda na kuapishwa kuwa Mbunge wa BJAM Mhe. Dkt. Kalinda, alikuwa Mkuu wa Kitivo cha Sheria katika Chuo Kikuu cha Rwanda. Mhe. Dkt Kalinda ameapishwa kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Celestine Kabahizi ambaye alijiuzulu Juni, 2015.

Aidha, Mhe. Leontine Nzeyimana, ameteuliwa kwa mara nyingine kuwa Waziri wa Wizara ya Masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kufuatia uchaguzi uliofanyika Mwezi Julai Nchini Burundi. Mhe. Nzeyimana ameiongoza Wizara katika nafasi hiyo tangu mwaka 2012. Mhe. Nzeyimana ana Shahada ya Uzamili katika Mahusiano ya Kimataifa, ambapo kabla alisoma Shahada ya Usimamizi wa Biashara katika Chuo Kikuu cha Tumaini Iringa, Tanzania aliyohitimu mwaka 2002.

MUSWADA WA SHERIA YA MIAMALA YA KIELEKTONIKI WA MWAKA 2014 WAPITISHWA



MUSWADA WA SHERIA YA MIAMALA YA KIELEKTONIKI WA MWAKA 2014 WAPITISHWA

Muswada wa Sheria ya Miamala ya Kielektoniki wa Jumuiya ya Afrika mashariki uliokuwa ukijadiliwa na Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (BJAM) katika vikao vyake vinavyoendelea Jijini Nairobi Kenya, Oktoba 9, 2015 lilipitisha muswada wa sheria ya miamala wa kielektoniki wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwa ni moja ya mikakati ya Jumuiya ya kutengeneza mazingira mazuri ya kufanya miamala ya biashara kwa mfumo wa digitali.

Moja ya sababu za msingi zilizokuwa zikitolewa na Wabunge wengi wakati wakichangia mjadala wa kupitishwa kwa Muswada wa sheria hiyo walisema Sheria hii itakuwa ni chachu ya ukuaji uchumi wa Nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki, kwa kuwa inalenga kukuza teknolojia ambayo itatumika kuendesha miamala ya kibiashara ya kieletoniki katika mazingira ya kisasa sambamba na kuboresha ufanisi na usalama kwa watumiaji wa huduma hiyo, pia itakidhi mahitaji ya sasa ya miamala ya kielectoniki katika biashara.

Mjadala juu ya muswada wa sheria hii uliahirishwa katika Mkutano wa kwanza wa Kikao cha Nne cha Bunge la tatu uliofanyika Agosti , 2015 Jijini Kampala, Uganda baada ya Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri Mhe. Dkt. Abdullah Saadala kulieleza Bunge hilo kuwa Muswada huo unahitaji kuboreshwa zaidi na wadau kabla haujapitishwa.

Baada ya kupitishwa kwa Muswada wa sheria hiyo Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki ambaye pia ni Naibu Waziri Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Abdallah Saadala alisema Wabunge walijadili Muswada huo wakiwa na sura moja wakizingatia faida ambazo Nchi wanachama zitanufaika nazo kutokana na sheria hiyo.

Tuesday 13 October 2015

Katibu Mkuu Bibi Joyce Mapunjo (kulia) akizungumza na Balozi anayeiwakilisha Nchi ya Switzerland katika Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Arthur Mattli (kushoto) alipoitembelea Wizara 12/10/2015.


Monday 5 October 2015

                       

                      JAMHURI YA MUUNGANO WA                            TANZANIA
WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


  MKUTANO WA PILI WA BUNGE LA JUMUIYA YA  AFRIKA MASHARIKI KUANZA                                                                                   LEO.

Mkutano wa pili, kipindi cha nne wa Bunge la tatu la Jumuiya ya Afrika Mashariki unaanza leo tarehe 5 Oktoba, 2015 Jijini Nairobi, Nchini Kenya, ukumbi wa Bunge la Nchi hiyo. Mkutano huu unatarajiwa kufanyika kwa siku 11, kuanzia tarehe 5 hadi 15 Oktoba 2015.

Mkutano huu unatarajiwa kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta siku ya jumanne tarehe 6 Oktoba, 2015.

Katika Mkutano huu, Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (BJAM) pamoja na mambo mengine litatumia vikao vyake kupokea na kujadili ripoti za kamati mbalimbali za Bunge na kujadili miswada mitatu ya kisheria. Miswada hiyo itakayo jadiliwa ni;

· Muswada wa sheria wa miamala ya elektoniki wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa mwaka 2014 (The EAC Electronic Transaction Bill 2014).

· Muswada wa Sheria ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wa kusimamia na kulinda Misitu wa Mwaka 2015 (The EAC Forests Management and Protection Bill 2015).

· Muswada wa Sheria ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wa kupunguza na kukabiliana na majanga (The East African Community Disaster Risk Reduction and Management Bill)

Katika Mkutano huu wa pili wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kulihutubia Bunge hilo tarehe 12 Octoba, 2015 na atatumia fursa hii kuliaga Bunge hilo.

                     
                                                 Imetolewa na,
                      Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.