Sunday 22 November 2015

BUNGE LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI LAANZA



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
   TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 
BUNGE LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI LAANZA 

Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki leo linatarajia kuanza vikao vyake Jijini Kigali, Rwanda. Mkutano huu watatu wa Bunge la tatu la Jumuiya ya Afrika Mashariki (BJAM) utafanyika kwa siku kumi na tatu (13) kuanzia leo Jumatatu Novemba 23, 2015 hadi Ijumaa Disemba 4, 2015. 

BJAM litaongozwa na spika wake Mhe. Daniel F. Kidega, na kufunguliwa na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame.

Bunge hili litakalofanyika kwa wiki mbili pamoja na mambo mengine litajadili misuada ya kisheria ifauatayo; 

· Musuada wa sheria ya kupunguza majanga ya mwaka 2013 (Disaster Risk Reduction Bill 2013.) 

· Musuada wa sheria ya Usiamamizi na Ulinzi wa Misitu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC Forestry Management and Protection Bill 2014) 

Musuada wa Sheria ya Misitu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki unalenga kukuza maendeleo ya misitu, ulinzi, uhifadhi, usimamizi na matumizi endelevu ya Misitu katika Jumuiya kwa manufaa ya vizazi vya leo na vijavyo. 

Mjadala wa Musuada wa Sheria ya Usimamizi na Ulinzi wa Misitu ya Mwaka 2014 uliahirishwa katika kikao cha Oktoba 2015 kilichofanyika Jijini Nairobi, kufuatia pendekezo la Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAM) Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe la kuliomba Bunge kuahirisha mjadala huo ili kuipa Tanzania muda wa kutosha wa kuandaa mapendekezo juu ya sheria hiyo. 

Musuada wa Sheria ya Kupunguza Majanga ya mwaka 2013 ya JAM inalenga kutoa mfumo wa kisheria ambao utatoa msaada kwa wahanga wa maafa yanayotokana na mabadiliko ya tabia Nchi na majanga ya asili sambamba na kulinda mazingira asilia katika Mtangamano na kusimamia mikakati itakayowekwa ili kupunguza athari za maafa. 

Aidha, BJAM katika vikao vyake linatarajia kupokea na kujadili ripoti zifuatazo; 

· Ripoti ya taarifa ya ukaguzi wa fedha za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2014 kutoka Kamati ya Hesabu. 

· Ripoti ya Warsha na Uhamasishaji kuhusu viwango vya Shirika la Viwango la Afrika(African Organization of Standardization) kutoka Kamati ya Kilimo, Maliasili na Utalii 

· Ripoti ya tathimini ya Vituo ya Utoaji huduma kwa Pamoja Mpakani vya Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Kamati ya Mawasiliano, Biashara na Uwekezaji. 

· Ripoti ya utekelezaji wa Maazimio na Maswali ya Baraza la Mawaziri na BJAM kutoka Kamati ya Sheria, Kanuni na Haki. 

Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki linafanya Mikutano yake kwa utaratibu wa Mzunguko miongoni mwa Nchi wanachama kama ilivyoainishwa kwenye Ibara ya 55 ya Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Aidha BJAM linakutana kwa Mwaka mara moja katika Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Arusha, Tanzania. 

Imetolewa na,
Katibu Mkuu,
Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Wednesday 18 November 2015

MKUTANO WA KUWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MIRADI INAYOFADHILIWA NA TMEA

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bibi Robi Bwiru akiwasilisha taarifa ya utekelezaji kwenye Mkutano wa 17 wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Miradi inayofadhiliwa na TMEA uliofanyika Hoteli ya Serena Jijini Dar 17/11/2015.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bw. Petro Lyatuu (kulia) akitoa taarifa kwenye Mkutano wa 17 wa wadau wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Miradi inayofadhiliwa na Shirika la TradeMark East Afrika uliofanyika Hoteli ya Serena Jijini Dar 17/11/2015.
Baadhi ya Wajumbe wakifuatilia kwa makini Mkutano wa 17 wa wadau wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inayofadhiliwa na Shirika la TradeMark East Afrika uliofanyika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam 17/11/2015.
Katibu Mkuu Bibi Joyce Mapunjo (kushoto) akifafanua jambo kwa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la TradeMark East Afrika (TMEA) Dkt. Josaphat Kweka kwenye Mkutano wa 17 wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inayofadhiliwa na TMEA 17/11/2015.
Mkurugenzi Msaidizi wa Miundombinu Bw. Abdillah Mataka (wa kwanza kushoto) akielezea jambo kwenye Mkutano wa 17 wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inayofadhiliwa na TMEA 17/11/2015
Katibu Mkuu Bibi Joyce Mapunjo (kushoto) akifafanua jambo kwa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la TradeMark East Afrika (TMEA) Dkt. Josaphat Kweka kwenye Mkutano wa 17 wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inayofadhiliwa na TMEA 17/11/2015.
Katibu Mkuu Bibi Joyce Mapunjo akifafanua jambo kwa awadau wa kwenye Mkutano wa 17 wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inayofadhiliwa na Shirika la TMEA uliofanyika Hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam 17/11/2015.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bw. Petro Lyatuu (katikati), Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bibi Robi Bwiru (kushoto), Mtaalamu Mshauri wa masuala ya M&E Bw. Michael Abila (kulia) wakifuatilia jambo wakati wa Mkutano wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Miradi inayofadhiliwa na Shirika la TradeMark East Afrika uliofanyika Hoteli ya Serena Jijini Dar 17/11/2015.
Katibu Mkuu Bibi Joyce Mapunjo (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la TradeMark East Afrika (TMEA) Dkt. Josaphat Kweka kwenye Mkutano wa 17 wa wadau wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inayofadhiliwa na TMEA Nchini 17/11/2015.
Baadhi ya Wajumbe wakifuatilia jambo kwenye Mkutano wa 17 wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inayofadhiliwa na Shirika la TradeMark East Afrika uliofanyika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam 17/11/2015.
Katibu Mkuu Bibi Joyce Mapunjo akifungua Mkutano wa 17 wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na Shirika la TradeMark East Afrika uliofanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam 17/11/2015.
Katibu Mkuu Bibi Joyce Mapunjo (katikati) akifurahia jambo wakati akiwakaribisha wajumbe (hawapo pichani) kwenye Mkutano wa 17 wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Miradi inayofadhiliwa na Shirika la TradeMark East Afrika uliofanyika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la TradeMark East Afrika Dkt. Josaphat Kweka.