Sunday, 31 January 2016

MHE. NAIBU WAZIRI DKT. SUSAN KOLIMBA ATEMBELEA KITUO CHA UTOAJI HUDUMA KWA PAMOJA MPAKANI HOLILI

Mhe. Naibu Waziri Dkt. Susan Kolimba (katikati) akiwa katika mazungumzo na Maafisa wa Kituo cha Kutolea Huduma kwa Pamoja  Holili.
Maafisa wa Kituo cha Kutolea Huduma Kwa Pamoja cha mpaka wa Holili wakimsiliza Mhe. Naibu Waziri Dkt.Susan Kolimba (hayupo pichani)
Mhe. Naibu Waziri Dkt. Susan Kolimba (kushoto) akizungumza na watendaji (hawapo pichani) wa Kituo cha Kutolea Huduma kwa Pamoja mpaka wa Holili
Msimamizi wa Kituo cha Kutolea  Huduma kwa Pamoja Mpakani Bw. A. Mwakalobo (kulia-aliyesimama) akitoa malezo kwa Mhe. Naibu Waziri Dkt. Susan Kolimba (wapili kushoto kati ya walioketi) juu ya ufanyaji kazi wa kituo hicho
Mhe. Dkt Susan Kolimba (kushoto) akiwa katika kituo cha kutolea huduma kwa pamoja (OSBP) mpaka  wa Holili, Kulia ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bw. Petro Lyatuu
Mhe.Naibu Waziri Dkt. Susan Kolimba (kulia) akiwa ameongozana na msimamizi wa Kituo cha Kutolea huduma kwa pamoja (One Stop Border Post) mpaka wa Holili alipotembelea kituo hicho 30/01/2016


ELIMU KWA UMMA NI MSINGI KATIKA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI- EALA

ELIMU KWA UMMA NI MSINGI KATIKA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI- EALA 

Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki(BJAM) ambalo linaeendelea na vikao vyake Jijini Arusha, terehe 28 Januari, 2016 waliendelea na mjadala kuhusu ripoti iliyowasilishwa kuhusu kibali cha ukaazi/kufanya kazi (work / residence permit) katiki Nchi wanachama za Afrika Mashariki. 

Katika mjadala huo kwa sauti ya pamoja Wabunge walisisitiza suala la elimu kwa umma kutiliwa mkazo kwa Nchi zote wanachama, wakichangia wabunge hao walisema suala la elimu kwa umma ni suala la Msingi sana kwani katika Mkataba wa uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kifungu cha 7 kinasema Jumuiya hii itakuwa ni Jumuiya ya watu na inayozingatia masoko “ The Community shall be people centered and Market driven” kwa kuzingatia hilo ni muhimu sana kwa wananchi kuelimishwa ili kuweza kuwa sehemu ya Jumuiya hii na kuweza kunufaika na matunda ya Jumuiya hii hasa ya Soko la pamoja. 

Wakiongea katika mjadala huo wabunge walisema wakati mwingine wanachi wanajikuta katika matatizo hasa wanapotoka Nchi moja kwenda Nchi nyingine ya Afrika Mashariki kwa sababu hawajui taratibu na makubaliano yaliyofikiwa katika maeneo mbalimbali ya ushirikiano katika Jumuiya. 

Katika kutekeleza Itifaki ya Soko la Pamoja kuna Mipaka, Soko la pamoja haimanishi kwamba kila kitu kitakuwa huru, kuna maeneo ambayo Nchi wanachama walikubaliana kushirikiana na wakati huohuo sheria na taratibu za Nchi mwanachama husika zinapaswa kuzingatiwa. Hivyo wananchi wanatakiwa kuelimishwa mipaka na makubaliano malimbali yaliyofikiwa katika Itifaki mbalimbali katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. 

Akichangia katika mjadala huo Mbunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa upande wa Tanzania Mhe. Shyrose Bhanji, alisisitiza Nchi wanachama kuchangamkia fursa za Soko la Pamoja la Afrika Mashariki 

“ Nashangaa ni Watanzania wangapi mfano wamechangamkia fursa ya kwenda kufundisha Lugha ya Kiswahili kwenye Nchi hizi za Afrika Mashariki? Ni wakati sasa umefika jitihada za kuhakikisha elimu kwa umma hasa kwa fursa zinazopatikana katika Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki inawafikia wananchi wote ili wananchi wengi waweze kupata fursa ya kufanya kazi katika Nchi Wanachama” alisisitiza Mhe. Shyrose. 

Katika mjadala huo wabunge walitilia mkazo suala la kuhuisha sheria mbalimbali za ndani ya Nchi wanachama ili masuala mbalimbali yaliyokubaliwa katika Itifaki ya Soko la Pamoja yaweze kutekelezeka, hasa kuhakikisha ada za vibali vya ukaazi/kufanya kazi zinahuishwa ili wananchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waweze kufanyakazi au kuishi katika Nchi wanachama. 

Wabunge hao wamehimiza Nchi wanachama kuhakikisha wanalipa kipao mbele swala la elimu kwa umma ili wananchi waweze kujua masuala mbalimbali katika Jumuiya, vilevile wametoa wito kwa wananchi wa Afrika Mashariki kuchangamkia fursa mbalimbali zinazopatikana katika Jumuiya hasa katika Soko la Pamoja wakati huohuo wakizingatia sheria na taratibu za Nchi husika kama ilivyo makubaliano katika Itifaki mbalimbali katika maeneo ya Ushirikiano.
Thursday, 28 January 2016

MHE. NAIBU WAZIRI AKIJIBU HOJA ZA WABUNGE

Mhe. Naibu Waziri Dkt. Susan  Kolimba (kushoto-aliyesimama) akijibu hoja za Wabunge katika Mkutano wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki unaondelea Jijini Arusha.

Wednesday, 27 January 2016

MHE. Dkt. SUZAN KOLIMBA ALA KIAPO BUNGE LA AFRIKA MASHARIKIMHE. Dkt. SUSAN KOLIMBA ALA KIAPO BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI.
Mhe. Naibu Waziri Dkt Susan Kolimba akila kiapo 26/01/2016

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa amekula kiapo leo katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, kiapo hiki kinamuwezesha kushiriki vikao vya Bunge kama Mbunge anayeingia kwa nafasi yake (Ex-Officio Member) hii ni kwa mujibu wa sheria namba 5 ya Sheria za Bunge hilo, kiapo hicho kilitolewa mbele ya Spika wa Bunge hilo Mhe. Daniel F. Kidega.


Baada ya kiapo Mhe. Dkt Susan alichukuwa nafasi yake kama mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri katika Kikao hicho. Akiongea baada ya kuchukuwa nafasi yake Mhe. Dkt. Kolimba amelihakikishia Bunge hilo kwamba Tanzania itahakikisha inashiriki kikamilifu katika hatua zote za Mtangamano ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa katika kuanzisha Jumuiya hii kwa faida ya WanaAfrika Mashariki. ‘Kama ilivyo kauli mbiu ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya “Hapa kazi tu”, sisi kama wenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki tunawahakikishia wanaafrika Mashariki tutaeenda kwa kasi ya Hapa kazi tu ili kuhakikisha Mtangamano huu unakuwa na faida kwa Wanaafrika Mashariki wote’ alisema Mhe. Dkt. Kolimba.


Aidha, katika hatua nyingine katika kikao hicho kutokana na ratiba, bunge lilikuwa linajadili musuada wa sheria ya kupunguza majanga ya mwaka 2013 (Disaster Risk Reduction Bill 2013). 

Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki Dkt. Susan A. Kolimba kwa niaba ya Baraza la Mawaziri aliomba musuada huo kutojadiliwa na kusogezwa mbele ili kulipa nafasi Baraza la Mawaziri kuweza kuboresha zaidi muswada huo, baada ya majadiliano wabunge waliridhia maombi ya Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri na Musuada huo utajadiliwa tena Machi, 2016 baada ya Baraza la Mawaziri la Afrika Mashariki kufanya maboresho.

Bunge la Afrika Mashariki ni chombo cha Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichoanzishwa chini ya Ibara ya 9 ya Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki( The Treaty for the Establishment of East African Community). Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki linafanya Mikutano yake kwa utaratibu wa Mzunguko miongoni mwa Nchi wanachama kama ilivyoainishwa kwenye Ibara ya 55 ya Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Aidha BJAM linakutana kwa Mwaka mara moja katika Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Arusha, Tanzania.

Mhe. Naibu Waziri Dkt. Susan Kolimba (mwenye Biblia mkononi) akila kiapo mbele ya Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki linaloendelea Jijini Arusha.
Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhe. Daniel F. Kidega (aliyesimama) akiendesha vikao vya Bumge hilo. 
Mhe. Naibu Waziri Susan Kolimba (katikati) akisindikizwa na baadhi ya Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki wa Tanzania, Mhe. Shy- Rose Sadrudin Bhanji (kushoto) na Mhe. Angela Charles Kizigha (kulia) wakati akienda kula kiapo mbele ya Bunge hilo.Monday, 25 January 2016

NAIBU WAZIRI MHE. SUZAN KOLIMBA AKUTANA NA SPIKA WA BUNGE LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI.

Naibu Waziri Mhe. Suzan Kolimba (kulia) akisalimiana na Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhe. Daniel Fred Kidega (kushoto) Jijini Arusha Januari 25, 2016.
Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) Mhe. Daniel Fred Kidega (katikati) akizungumza na waandishi wa habari Jijini Arusha, wengine ni Mhe. Abdulla Mwinyi (kushoto -Mbunge kutoka Tanzania) na Mhe. Hafsa Mossy (kulia-Mbunge wa Burundi) 
Mhe. Naibu Waziri Dkt. Suzana Kolimba (aliyevalia vitenge) akimsikiliza mfanyakazi wa Bunge la Afrika Mashariki Bw. Asheri Wimile (kulia) alipoenda kumsalimia. Kushoto ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bw. Petro Lyatuu.
Naibu Waziri Mhe. Suzan Kolimba (kulia) na Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhe. Daniel Fred Kidega (kushoto) wakifurahia jambo.
Naibu Waziri Mhe. Dkt. Suzan Kolimba (kulia) akiwa katika mazungumzo na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Mhe. Daniel Fred Kidega (kushoto) Januari 25, 2016.


MWINYI KUWA MWENYEKITI WA JOPO LA UANGALIZI WA UCHAGUZI UGANDA.

MWINYI KUWA MWENYEKITI WA JOPO LA UANGALIZI WA UCHAGUZI UGANDA.


Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dk. Richard Sezibera amemwomba Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mhe. Al Hassan Mwinyi kuwa Mwenyekiti wa Jopo la waangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Nchini Uganda.

Dr. Sezibera alisema hayo alipomtembelea Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dk. Balozi Aziz Mlima ofisini kwake kwa lengo la kumuelezea nia ya mazungumzo yake na Rais Mwinyi ikiwa ni pamoja na masuala mengine ya Jumuiya kuhusu Mkutano Mkuu wa Kilele wa Viongozi Wakuu wa Jumuiya.

Aidha Dk. Sezibera katika mkutano wake na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo amesema Rais Mwinyi amekubali ombi hilo na kumuomba Katibu Mkuu wa Wizara kusaidia kutafuta msaidizi wa Rais Mwinyi atakaye kuwa msemaji mzuri ukizingatia kipindi cha uchaguzi vyombo vya Habari huwa na mambo mengi yakufuatilia katika uchaguzi utakaofanyika mapema mwezi ujao.

Pamoja na maelezo yake kuhusu masuala ya Uchaguzi Nchini Uganda Dk. Sezibera alizungumzia kuhusu kufanyika kwa Mkutano wa Baraza la Mawaziri na Mkutano wa Kilele wa Viongozi Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaotarajia kufanyika Jijini Arusha tarehe 29 mwezi wa pili na kumueleza kuwa utakuwa mzito sana na wa aina yake kufuatia mkutano huo kuunganishwa na mkutano mwingine muhimu wa masuala ya bajeti ya Jumuiya.

Pamoja na Mambo mengine pia agenda za Mkutano Mkuu huo zitaangalia masuala ya maombi ya Sudan ya Kusini kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki, masuala ya Jumuiya kufikia shirikisho la kisiasa, kuzindua hati ya kusafiria ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yenye hadhi ya kimataifa pamoja na mapitio ya muundo wa Sekretariati ya Jumuiya. 

Mkutano huu uliotakiwa ufanyike mwishoni mwa mwaka jana kwa mujibu wa kalenda ya kazi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliahirishwa kufuatia muulingiliano wa ratiba za uchaguzi uliokuwa ukiendelea miongoni mwa nchi wanachama ikiwemo Tanzania, na badala yake utafanyika Februari 29, 2016.

KATIBU MKUU BALOZI DKT. AZIZ MLIMA AKUTANA NA KATIBU MKUU WA SEKRETARIATI YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

Kutokea kushoto ni Mkurugenzi wa Siasa, Ulinzi na Usalama Bw. Stephen Mbundi, Mhandisi John Kiswaga, na Bw. Antony Ishengoma (wakwanza kulia) wakifuatilia mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea
Katibu Mkuu wa Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Dkt. Richard Sezibera akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu Balozi Dkt. Aziz Mlima.
Katibu Mkuu Balozi Dkt. Aziz Mlima (kulia) akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Dkt. Richard Sezibera alipo mtembelea ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.

Friday, 22 January 2016

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE, USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI, KIKANDA NA KIMATAIFA
                                                              
Description: Description: Coat of Arms
                         

Simu ya maandishi: ‘MEAC’
Simu Na. 022-2126827, 2126830, 2126823
Fax: 022 – 2126651/2120488
Barua Pepe: ps@meac.go.tz
Tovuti: www.meac.go.tz

NSSF Waterfront Ghorofa ya 5
35 Barabara ya Edward Sokoine
S.L.P 9280,
11467 DAR ES SALAAM,
Tanzania.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MKUTANO WA NNE WA BUNGE LA TATU LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUANZA JIJINI ARUSHA

Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki linatarajia kuanza mkutano wake Jijini Arusha, Tanzania. Mkutano huu wanne wa Bunge la tatu la Jumuiya ya Afrika Mashariki (BJAM) utafanyika kwa siku kumi na mbili (12) kuanzia leo Jumatatu Januari 24, 2016 hadi Ijumaa Februari 5, 2016. 

BJAM ambalo litaongozwa na spika wake Mhe. Daniel F. Kidega, katika vikao vyake litajadili taarifa kutoka kamati mbalimbali zenye mapendekezo kuhusu hatua mbalimbali za mtangamano kutoka kwa wadau sambamba na kujadili taarifa za kamati zifuatazo; 

· Taarifa ya Kamati ya Malengo ya Pamoja inayozungumzia kuhusu maombi ya vibali vya kazi na uraia, kufuatia mapendekezo ya Shirikisho la Wafanyakazi la Afrika Mashariki na Chama cha Waajiri Afrika Mashariki. 

· Kupokea na kujadili taarifa kutoka Kamati ya Sheria na Kinga kuhusu mapendekezo ya maboresho na marekebisho ya kanuni mbalimbali za BJAM. 

Katika hatua nyingine wakati wa Mkutano huu wa Bunge kutakuwa na zoezi la kuapishwa kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Dkt. Suzan Kolimba ili aweze kushiriki katika Vikao vya Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki. 

Aidha, BJAM linatarajia kupokea na kujadili Musuada wa kupunguza majanga ya mwaka 2013 (Disaster Risk Reduction Bill 2013). 

Vilevile, suala la mgogoro wa kisiasa wa Nchini Burundi unatarajiwa kuwa sehemu ya mjadala katika Mkutano huu wa nne wa Bunge hilo. Kamati ya Bunge ya Masuala ya Kikanda na Usuluhishi wa migogoro itamalizia na kuwasilisha taarifa iliyoipokea kutoka Chama cha Wanasheria cha Umoja wa Afrika inayohusu hali ya kisiasa Nchini Burundi. 

Katika BJAM Tanzania inawakilishwa na Wabunge Tisa; Mhe. Charles Makongoro Nyerere ambaye ni Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki, Mhe. Issa Twaha Taslima ambaye ni Katibu, wengine ni Mhe. Abdullah Ally Hassan Mwinyi, Mhe. Shy-Rose Sadrudin Bhanji, Mhe. Adam Omar Kimbisa, Mhe. Angela Charles Kizigha, Mhe. Bernard Musomi Murunya, Mhe.Perpetua Kessy Nderakindo na Mhe. Maryam Ussi Yahya 

Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki linafanya Mikutano yake kwa utaratibu wa Mzunguko miongoni mwa Nchi wanachama kama ilivyoainishwa kwenye Ibara ya 55 ya Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Aidha BJAM linakutana kwa Mwaka mara moja katika Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Arusha, Tanzania. 

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Mambo ya Nje,Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa
Dar es Salaam, Januari 23, 2016

Tuesday, 19 January 2016

Tanzania: Tupo tayari kushiriki katika Mazungumzo ya Burundi


Tanzania: Tupo tayari kushiriki katika Mazungumzo ya Burundi.

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Maiga akizumgumza na waandishi wa habari mwishoni wa wiki alisema Tanzania ipo tayari kushiriki katika mazungumzo ya kuiletea amani Burundi kadri itakavyo amliwa na Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki unaotarajiwa kufanyika siku za karibuni.

Katika Mkutano huo na waandishi wa habari ambao pia alishiriki Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi Mhe. Alain Aime Nyamitwe, Waziri Mhe. Balozi Dkt Maiga ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki alisema “nimempokea Waziri wa Burundi leo, sababu ya ujio wake ni kutoa ishara na uthibitisho kuwa Burundi iko tayari kutushirikisha katika kutafuta suluhu na amani tukiwa kama wenyekiti, ni jambo la kufurahisha pia kuona mazungumzo ya amani yanaendelea baina ya Warundi wenyewe, na kwa kuhusisha Mataifa mengine katika kuleta amani”. 

Aidha kwa upande wake Waziri wa mambo Mambo ya Nje wa Nchini Burundi Mhe.Alain Aime Nyamitwe katika Mkutano huo alisema Burundi ikotayari kuendelea na mazungumzo ya kuleta amani nchini humo kufuatia changamoto za kiusalama zinazo ikabili Nchi hiyo baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika Julai 21, 2015.

“Hali ya Burundi ni salama, tunakabiliwa na changamoto chache za kiusalama katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Bujumbura lakini ukienda maeneo ya vijijini hali ni shwari kabisa na wananchi wanaendelea na kazi zao za kila siku kama kawaida na Serikali inajitahidi kufanya kila linalowezeakana kuhakikisha changamo hizi za kiusalama zinatatuliwa mapema iwezekanavyo” alisema Mhe. Nyamitwe. 

Aliongeza kusema Mazungumzo ya ndani ya Nchi na Msuluhishi yanaendelea pia kwa kuhushikisha makundi mbalimbali ya kijamii zikiwemo asasi za kiraia, viongozi wa dini na wananchi wote kwa ujumla.


Mhe. Nyamitwe aliwasili Jijini Dar es Salaam Ijumaa tarehe 15/01/2016 kumtembelea Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Maiga ambapo baada ya mazungumzo kwa pamoja waliongea na vyombo vya habari katika Mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi mdogo wa Mikutano wa Wizara. Kwa wakati huu Tanzania ni Mwenyeki wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

WIZARA YAFANYA KIKAO NA WABUNGE WA AFRIKA MASHARIKI

Mhe. Waziri Balozi Dkt. Augustine Mahiga (wakwanza kulia), akizungumza na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki wa Tanzania wakati wa kikao kati ya Wizara na Wabunge hao.
(Kulia-kushoto) Ni Mhe. Waziri Balozi Dkt. Augustine Mahiga, Naibu Waziri Mhe. Dkt. Suzan Kolimba, wakibadilishana mawazo na Waheshimiwa Wabunge wa Afrika Mashariki, Mhe. Charles Makongoro Nyerere, Mhe. Shy-Rose Sadrudin Bhanji, Mhe. Angel Charlers Kizigha na Mhe. Bernard Musomi Murunya. 


Monday, 18 January 2016


Mhe. Waziri Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) na Mhe. Naibu Waziri Dkt. Suzan Kolimba (kushoto-walioketi) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki na baadhi ya watendaji wa Wizara.

Saturday, 16 January 2016

HABARI KATIKA PICHA

Waziri wa Mambo ya Nje wa Nchini Burundi Mhe. Alain Aime Nyamitwe (kushoto) akifanunua jambo kwa waandishi wa habari wakati akizungumza na waandishi hao Jijini Dar es Salaam, Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Maiga.
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Maiga (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)  katika ukumbi mdogo wa mikutano wa  Wizara, Jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Nchini Burundi Mhe. Alain Aime Nyamitwe 15/01/2016.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Nchini Burundi Mhe. Alain Aime Nyamitwe (kushoto) akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) alipomtembelea Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa wa Nchini Tanzania Mhe. Balozi Augustine Maiga (katikati), kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasilino  Serikalini  Wizara ya Mambo Nje Bi. Mindi Kasiga 15/01/2016,
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Maiga (kulia) akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Nchini Burundi Mhe. Alain Aime Nyamitwe (kushoto) alipomtembea Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam 15/01/2016. 
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Maiga (kulia) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Nchini Burundi Mhe. Alain Aime Nyamitwe (kushoto) alipomtembea Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam 15/01/2016.