Friday 29 May 2015

(Kulia–kushoto) Naibu katibu Mkuu  Bw. Amentius Msole, Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu ya Kiuchumi na Huduma za Kijamii Bw. George Lauwo na Mkurugenzi Mkazi wa TMEA Bw. Josaphati Kweka wakifuatilia uwasilishwaji wa hotuba ya bajeti Bungeni mjini Dodoma 29/05/2015

Katibu Mkuu Bi. Joyce Mapunjo (katikati) akifuatilia jambo wakati wa usilishwaji wa hotuba ya makadilio ya mapato na matumizi kwa Mwaka 2015/2016 Bungeni Mjini Dodoma leo 29/05/2015.

Waziri Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akisoma hotuba ya Makadilio ya mapato na matumizi kwa Mwaka 2015/2015 Bungeni Mjini Dodoma leo 29/05/2015.

Waziri Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) na  Naibu Waziri Mhe. Dkt. Abdulla Saadala (kulia) wakifuatilia  kikao cha uwasilishwaji wa hotuba ya makadilio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2015/2016 Bungeni Jijini Dodoma 29/05/2015.

Monday 4 May 2015

(Kulia-kushoto) Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu Bi. Vedastina Justinian, Bi. Mamertha Josiah (Katibu Muhtasi) na Ponslaus Makua (Mhasibu) wakiwa kwenye maadhimisho ya sherehe ya siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Kitaifa  katika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza 01/05/2015. Bi. Mamertha Josiah (katikati) alitunukiwa tuzo ya kuwa mfanyakazi bora wa Wizara 2014/2015.
1 Mei, kila mwaka ni siku ya maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani. Pichani ni Wafanyakazi wa Wizara walipojumuika na Wafanyakazi wengine kwenye maadhimisho ya sherehe hiyo iliyofanyika kimkoa katika uwanja wa Taifa Dsm 1 Mei, 2015.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utawala na Usimamizi Rasimali Watu Bw. Hamid H. Mbegu (katikati msatari wa mbele) akiwa na Wafanyakazi wengine wa Wizara katika maandamano ya sherehe ya kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani iliyofanyika Kimkoa katika uwanja wa Taifa Dar-es-Salaam 01/05/2015
Watumishi wa Wizara wakiwa katika sherehe ya maadhimisho ya Sherehe ya Siku ya Wafanyakazi Duniani iliyofanyika kimkoa katika Uwanja wa Taifa Dar-es-Salaam Mei 1, 2015
Watumishi wa Wizara wakiwa katika hali ya furaha wakati wa maandamano ya kuadhimisha sherehe ya siku ya Wafanyakazi Duniani iliyofanyika kimkoa katika Uwanja wa Taifa Dsm 1 Mei, 2015.


1 Mei, kila mwaka ni siku ya maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani. Katika picha ni Wafanyakazi wa Wizara walipo jumuika na Wafanyakazi wengine kwenye maadhimisho ya sherehe hiyo iliyofanyika kimkoa katika uwanja wa Taifa Dar-es-Salaam 1 Mei, 2015.