Monday 29 February 2016

HABARI PICHA; UZINDUZI WA KITUO CHA UTOAJI HUDUMA KWA PAMOJA MPAKANI HOLILI (OSBP)

Mhe. Waziri Balozi Dkt. Mahiga (wakwanza kushoto) akikata utepe wa kuashiria kufunguliwa rasmi kwa Jengo la OSBP la Holili.
Mhe. Waziri Balozi Dkt. Mahiga na Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki wa Kenya Mhe. Phillis Kandie (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja  na viongozi wengine kutoka Nchi Wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki 
Mhe. Waziri (katikati) akitembelea Jengo la OSBP kwa upande wa Kenya Taveta ambapo alifanya uzinduzi rasmi wa Jengo hilo.
Mhe. Waziri akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Jengo.
Mhe.Waziri wa tatu kutoka kushoto akifuatiwa na Waziri wa Kenya anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Phillis Kandie wakielekea upande wa Tanzania Holili kutoka Taveta kwa ajili ya ufunguzi rasmi wa Jengo la OSBP la Holili, wengine katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dr. Richard Sezibera kushoto kwa Mhe. Waziri.
Mhe. Waziri  Balozi Dkt. Augustine Mahiga (mwenye kipaza sauti mkononi) akizingumza na vyombo vya habari baada ya uzinduzi wa kituo cha utoaji huduma kwa pamoja (OSBP) cha Holili, Kulia ni Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki wa Kenya Bi. Kandie.
Mhe. Waziri Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki wa Nchini Kenya Bibi Phillis Kandie walipo kutana Jijini Arusha kabla ya uzinduzi wa Kituo cha kutoa Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) Holili.
Mhe. Waziri Balozi Dkt. Mahiga na Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki wa Nchini Kenya Mhe. Phillis Kandie wakijadili jambo.

Sunday 28 February 2016

KITUO CHA HOLILI CHAZINDULIWA RASMI

Kituo cha Holili chazinduliwa rasmi

Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanaoshughulilikia masuala yanayohusika na Vituo vya kutoa huduma kwa pamoja Mipakani wamezindua rasmi kituo cha Holili/Taveta katika mpaka wa Tanzania na Kenya, Kituo hicho kilizinduliwa rasmi tarehe 27 Februari, 2016
Mhe. Waziri akikata utepe wa kuashiria kufunguliwa rasmi kwa Jengo la OSBP la Holili.

Dhana ya Vituo vya Utoaji Huduma kwa Pamoja Mipakani ni dhana ya kisasa inayohusu Nchi zinazopakana, kutoa huduma, uwezeshaji na udhibiti kama forodha, uhamiaji, usalama na afya kwa kushirikiana. Hivyo, abiria au msafirishaji bidhaa halazimiki kusimama na kukaguliwa au kukamilisha taratibu za udhibiti sehemu mbili tofauti wakati wa kutoka kwenye nchi moja na wakati wa kuingia nchi nyingine. Hatua hii inawezesha Idara, Taasisi na Wakala kutoka Tanzania na Nchi jirani zinazotoa huduma na udhibiti mpakani kufanya kazi kwa pamoja na hivyo kupunguza muda wa kukaa mpakani na kuondoa vikwazo visivyo vya kiforodha. 
Kituo hichi kimejengwa kwa gharama zinazokadiliwa kuwa kiasi cha dola za Kimarekani 12 millioni ambao ni msaada kutoka kwa wahisani wa TradeMark East Africa (TMEA).

Kituo hiki kimefunguliwa rasmi kwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Waziri wa Kazi na Masuala ya Afrika Mashariki kutoka Kenya Bi. Phillis Kandie. 

Akiongea katika ufunguzi huo Mhe. Balozi Dkt. Mahiga alisema, “inafurahisha kuona maafisa wa pande mbili wakifanya kazi kwa ushirikiano, hii hainoeshi ushirikiaono tu bali inadhihirisha umoja na udhihirisho wa kauli mbiu ya Jumuiya ya ‘Watu wamoja, hatima moja – one people one destiny’. Hivyo nawasihi watu wetu wa Kilimanjaro na Taveta kutumia fursa hii kikamlifu”. 

Mhe. Waziri alisema Tanzania inathamini mchango wa Kituo hiki kwa kukuza biashara kati ya Tanzania na Kenya na kudhihirisha hilo Tanzania tayari imeridhia muswada wa kuongoza vituo hivi “OSBP Bill”. 

Vituo hivi vitasaidia kupunguza muda hivyo kupunguza gharama za kufanya biashara kwa wafanyabiashara, wakulima na wasafirishaji kutoka Nchi moja mwanachama kwenda Nchi nyingine.

Akiongeza alisema barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi inayotarajiwa kuzinduliwa tarehe 3 Machi,2016 itaongeza biashara ya mipakani na kuchochea ujirani mwema kati ya Tanzania na Kenya.

Mhe. Alisema kinachofuata ni kuwajengea uwezo watendaji wa kuendesha vituo hivi ili waweze kutoa huduma kwa ufaanisi.

Akiongea katika ufunguzi huo Mhe. Kandie alisema pamoja na kuwawezesha wakulima na wafanyabiashara kutoka Kaskazini mwa Tanzania kwenda soko la Kenya, Kituo cha Holili/Taveta kitasaidia kuongeza mahusiano na umoja. “Nimefuraishwa na hatua ya ujenzi wa Barabara ya Taveta-Mwatate-Voi, ambayo imefikia 75%, na inatarajiwa mwisho wa mwaka huu kazi hii itakamilika na hivyo watu wa Taveta na Kaskazini mwa Tanzania watasafiri kwenda Mombasa na sehemu nyingine za Kenya bila matatizo”

Mhe. Kandie alisistiza kwamba vikwazo visivyo vya kiforodha ni tatizo na alisema serikali ya Kenya kwa kushirikiana na Nchi nyingine Wanachama wanajitahidi kutafuta njia mbalimbali za kuondoa vikwazo hivyo ili kufanya Jumuiya hii iwe ya kiushindani na kuvutia zaidi.

Akiongea katika ufunguzi huo Katibu Mkuu wa Jumuiya Dkt. Sezibera alisema Holili/Taveta ni kituo cha kwanza kuzinduliwa kati ya vituo (8) vilivyojengwa katika mipaka ya Nchi wanachama na vimekamilika vinasubiria kufunguliwa rasmi, alisema “ Jumuiya ya Afrika Mashariki iligundua kuwa uchumi wa Nchi hizi wanachama unategemeana hivyo njia nzuri ya kufanyakazi pamoja ni kupunguza gharama za kufanya biashara”. 

Mr. Theo Lyimo, Mkurugenzi wa Vituo hivi kwa upande wa TMEA akiongea kwenye hafla hii aliwashukuru wahisani ambao wamesaidia mradi huu, wahisani hao ni - DFID, Canada, USAID and the World Bank.

“ Holili/Taveta ni kati ya vituo 15 Afrika Mashariki na Sudan ya Kusini vilivyojengwa kupitia ufadhili wa mradi wa TMEA, tumewekeza kiasi cha dolla za Kimarekani 117 million kinachofurahisha ni kwamba kati ya dolla 1 tuliyowekeza inatarajiwa kuleta dolla 30,” alisema Bw. Lyimo. 

Hafla hii ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka Tanzania na Kenya na hafla hii ilifanyikia kwa upande wa Tanzania - Holili.


Wednesday 24 February 2016

TAASISI YA MAENDELEAO YA WANAWAKE YA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI WAKUTANA NA WADAU JIJINI DAR ES SALAAM

Wajumbe wakifuatilia Mkutano
Mkurugenzi wa Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji Bw. Bernard Haule akiwasilisha mada kwenye Mkutano kati ya Taasisi ya Maendeleo ya Wanawake ya Ukanda wa Afrika Mashariki na Wadua uliofanyika katika Hoteli ya Blue Pearl Jijini Dar es Salaam  Februari 23, 2016.
Baadhi ya Wadau (Wanawake wajasiriamali) wakifuatilia Mkutano kwa Makini wakiwa na bidhaa zao mezani.
Mkurugenzi Msaidizi wa Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji Bw. Bernard Haule (kulia) akifuatilia jambo katika wakati wa mkutano kati ya Taasisi ya Maendeleo ya Wanawake ya Ukanda wa Afrika Mashariki na Wadau uliofanyika katika Hoteli ya Blue Pearl Jijini Dar es Salaam  Februari 23, 2016







SEKRETARIATI YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YATANGAZA NAFASI ZA KAZI



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE, USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI, KIKANDA NA KIMATAIFA

TAARIFA MUHIMU KWA UMMA

Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki imetangaza nafasi kumi (10) za kazi kupitia mtandao wake www.eac.int tarehe 19/02/2016. Kati ya nafasi hizo, nafasi tano (5) ni za kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki na nafasi tano (5) ni kutoka Tume ya Ushindani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (The EAC Competition Authority).

Maombi ya kazi hizo yanatakiwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambapo tarehe ya mwisho kuwasilisha maombi hayo kwa nafasi za Registrar, Deputy Registrar, Mergers and Acquisitions,Deputy Registrar, Monopolies and Cartels, Accounts Assistant na Senior Personal Secretary ni tarehe 13/03/2016. Kazi hizi ni za mkataba kwa kipindi cha miaka mitano (5) na kurudiwa mara moja kwa kipindi kingine cha miaka mitano kutegemea utendaji kazi wa mtumishi husika. Aidha tarehe ya mwisho ya kuwasilishwa maombi ya na nafasi za Accounts Assistant,Principal Research Fellow,Research Assistant, Senior Research Fellow na EAC Quality Management System (QMS) Focal Officer ni tarehe 18/03/2016. Nafasi hizi za mkataba kwa muda wa mwaka mmoja (1) na utarudiwa kutokana na utendaji kazi wa mtumishi pamoja na upatikanaji wa fedha.

Kwa maelekezo zaidi kuhusu utaratibu wa kuomba, kuwasilisha maombi na maelezo ya ziada tafadhali tembelea tovuti ya Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki : www.eac.int. au kupitia link; bofya hapa

Wizara inapenda kuwaarifu na kuwahamasisha Watanzania wenye sifa stahiki waweze kuomba kazi hizi ili kuongeza ushiriki na uwakilishi wa Tanzania katika Ajira za Jumuiya na hivyo kushiriki ipasavyo katika maamuzi mbalimbali yanayohusu nchi yetu katika Jumuiya.

Watanzania watakaopenda kuwasilisha maombi ya kazi hizo wawasiliane na Wizara hii kupitia Idara ya Utawala kwa maelekezo zaidi kabla hawajatuma maombi yao.

Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa
Februari 24, 2016.




Saturday 20 February 2016

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE, USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI, KIKANDA NA KIMATAIFA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Wizara imepata taarifa zisizo na ukweli zinazoenezwa na kusambazwa na watu wasiokuwa na nia njema kwa Wizara na Serikali kwa ujumla, kuwa Wizara iliyokuwa ya Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki iliendesha zoezi la kukusanya wasifu(CV) za Wafanyakazi wake kwa lengo la kuwafukuza kazi. 

Wizara imesikitishwa na inalaani vikali uvumi wa taarifa hizi na inakanusha kuwa taarifa hizi hazina ukweli wowote.

Zoezi la kukusanya CV za watumishi ni zoezi la kawaida kwa waajiri na hufanyika 

Mara kwa mara kwa lengo la kuhuisha sifa na uzoefu wa watumishi wanazopata wakiwa kazini ambapo hatimaye huwekwa kwenye majalada yao binafsi, mwajiri anapaswa kuhakikisha jalada la kila mtumishi lina taarifa zinazoeenda na wakati, hivyo zoezi hili lilifanyika kwa lengo la kuhuisha taarifa za watumishi wa Wizara kama ilivyoelekezwa na mwajiri na si vinginevyo.

Wizara inapenda kutoa ufafanuzi kuwa CV si miongoni mwa nyaraka zinazohitajika katika kumfukuza kazi mtumishi bali mtumishi anafukuzwa kazi kwa kukiuka sheria, kanuni na taratibu za kiutumishi ambapo taratibu maalumu za kinidhamu hufuatwa. Katika kipindi husika Wizara haina mtumishi anayetuhumiwa kwa kosa la kinidhamu linaloweza kupelekea kufukuzwa kazi, hivyo taarifa hizi hazina ukweli wowote.

Aidha, Wizara inakemea vikali watu wenye tabia ya kutoa taarifa zisizo na ukweli na zenye kupotosha umma. Vilevile Wizara inapenda kuwaasa wananchi kuheshimu sheria na taratibu za Nchi sambamba na kutoeneza taarifa zinazotokana na vyanzo visivyokuwa rasmi au zisizothibishwa na mamlaka husika, kwa kuwa kufanya hivyo ni kukiuka sheria na taratibu za Nchi.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.
19 Februari, 2016


Tuesday 16 February 2016

MKUTANO WA NANE (8) WA WATAALAM WA ENEO HURU LA BIASHARA YA UTATU (COMESA-EAC-SADC)

Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kikanda Balozi Innocent Shio akisalimiana na Mwenyeki wa Mkutano. 
Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kikanda Balozi Innocent Shio (kulia) akizungumza katika Mkutano wa Nane, ngazi ya wataalam wa eneo huru la Biashara ya Utatu, kushoto ni Mwenyekiti wa Mkutano huo.
Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kikanda Balozi Innocent Shio akifungua Mkutano wa Nane (8) ngazi ya wataalam wa eneo huru la biashara ya utatu (COMESA-EAC-SADC) unaofanyika katika Hoteli ya White Sand Jijini Dar es Salaam.







Wednesday 10 February 2016

MHE. NAIBU WAZIRI DKT. SUSAN KOLIMBA AKUTANA NA WABUNGE WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (EALA) ARUSHA

Mhe. Naibu Waziri (wa tatu kulia) akiongea na Wabunge wa Afrika Mashariki kwa upande wa Tanzania kabla ya kuingia kwenye kikao cha Bunge, kulia kwake ni Mhe. Nderakindo Kessy, Mhe. Makongoro Nyerere, Mhe. Maryam Yahya na Mhe. Shyrose Bhanji na kulia kushoto kwake ni Mhe. Angela Kizigha akifuatiwa na Mhe. Bernard Murunya anayeandika ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango.
Mwenyekiti wa Kamati ya Masuala ya Mtangamano na Utatuzi wa Migogoro Mhe. Abdullah A. Mwinyi akiwasilisha ripoti ya kamati hiyo kusuhu changamoto za utekelezaji wa Soko la Pamoja, kulia kwake ni Mhe. Spika wa Bunge la EALA Mhe. Daniel Kidega aliekaa kiti cha peke yake na wengine ni waandishi wa Bunge .
Mhe. Dkt Susan Kolimba, Naibu Waziri Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa akimpongeza Naibu Waziri Mkuu wa tatu na Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki Uganda Mhe. Kirunda Kivejinja baada ya kuapishwa hapo jana kuwa Mjumbe maalum wa Bunge la Afrika Mashariki, katikati ni Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki Burundi Mhe. Leontine Nzeyimana


TANZANIA YAPONGEZWA UONDOAJI WA VIKWAZO VISIVYO VYA KIFORODHA

Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki linaendelea na vikao vyake Jijini Arusha, Vikao hivyo vilianza tarehe tarehe 25 Januari, 2016 na Bunge hilo linatarajia kukamilisha shughuli zake tarehe 4 Februari, 2016. 

Katika kikao cha tarehe 02 februari, 2016 Bunge pamoja na mambo mengine lilijadili ripoti ya Kamati ya Bunge la Afrika Mashariki ya Masuala ya Mtangamano na Utatuzi wa Migogoro, ripoti hiyo iliyozungumzia Changamoto za kiusalama za utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja katika Ukanda wa Kati wa Usafirishaji( Central Corridol). 

Akiwasilisha taarifa, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Abdullah Ally Hassan Mwinyi Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kwa upande wa Tanzania, alisema kamati hii ilitembelea Ukanda huu na kukutana na wadau mbalimbali na kwa kiasi kikubwa walitembelea Tanzania kwa kuwa kwa takribani 90% ya Ukanda huu iko upande wa Tanzania.

Wakiongea kwa wakati tofauti wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki wameipongeza Tanzania kwa kufanya vizuri katika utekelezaji wa Umoja wa forodha na Soko la Pamoja, mafanikio haya ni kutokana na kazi nzuri inayofanywa na Kamati ya Kitaifa ya Ufuatiliaji wa kuondoa Vikwazo visivyo vya Kiforodha (National Monitoring Committee on elimination of NTBs) na Kamati ya Kitaifa ya Utekelezaji wa Soko la Pamoja (National Common Market Implementation Committee).

Kamati ya uondoaji Vikwazo visivyo vya kiforodha hadi Septemba,2015 imeweza kufanikisha kushughulikia jumla ya Vikwazo 87 kwa mara moja na ni vikwazo 18 tu ndio havijatatuliwa, kupunguza vizuizi vya barabarani katika Ukanda wa kati ( Road blocks) kutoka 56 hadi 6, Vizuizi hivyo vilivyobaki ni Vigwaza(Pwani), Mikese ( Morogoro), Nala(Dodoma), Njuki (Singida), Mwendakulima (Shinyanga) na Nyakahura (Kagera), kuweza kutoa jumla ya hati ya uasilia wa bidhaa( Certificates of Origin) 47,2333 kutoka July,2010 hadi June, 2015 na kuweza kuhamasisha wafanyabiashara wa ndani kutumia namba maalum za utambuzi wa bidhaa ( BARCODEs).

Kamati hii imepongeza ufanisi wa Mizani ya Vigwaza kwa kuwa na Teknologia ya Kisasa ambayo imeweza kupunguza muda wa kukagua mizigo na hivyo kuwapunguzia kero wasafirishaji, na Mizani za aina hizo zinatarajiwa kuwekwa katika kituo cha Manyoni (Singida) na Nyakanazi (Kagera) ili kuweza kubaki na Vituo vya Ukaguzi vitatu tu kwa upande wa Ukanda wa Kati.

Katika hatua nyingine Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhe. Daniel Kidega, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya hasa katika kuhakikisha ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam ambayo amesema ni kitovu cha Usafirishaji katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Spika huyo amesema wanaafrika Mashariki wanajivunia kwa kazi yake nzuri anayofanya na kwa kipindi kifupi ameweza kuwa Rais wa mfano katika Ukanda wa Afrika Mashariki. 

Wabunge katika hatua nyingine wamesisitiza umuhimu wa elimu kwa umma ili kuwawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika hatua mbalimbali za Mtangamano. Utekelezaji wa hatua hizi zote za Mtangamano utakuwa na mafanikio iwapo wananchi wa Afrika Mashariki watashirikishwa katika kila hatua kama Mkataba wa uanzishwaji wa Jumuiya unavyobainisha katika kifungu cha 7.