Sunday 17 July 2016
Thursday 23 June 2016
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki waadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma
Watumishi wakimsikiliza Katibu Mkuu Balozi Dkt. Aziz P Mlima (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma |
Watumishi wakimsikiliza Katibu Mkuu Balozi Dkt. Aziz P Mlima (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma |
Waliosimama ni Watumishi wapya waliojiunga na Wizara hivi karibuni wakitambulishwa wakati wa Mkutano wa maadhimisho ya Wiki ya utumishi wa umma |
Monday 20 June 2016
MHE. WAZIRI BALOZI DKT. MAHIGA AKUTANA NA RAIS WA SERIKALI YA ZANZIBAR MHE. DKT. SHEIN
Rais wa Serikali ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Dkt. Ali Mohamed Shein (kulia) akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) aliotembelea Ikulu |
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi (kulia) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. |
Friday 17 June 2016
Uhuru wa kufanya biashara ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Uhuru wa kufanya biashara ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuwajulisha wafanyabiashara wa Tanzania na wananchi wote kwa ujumla kuwa wanaweza kutumia fursa za biashara zinazopatikana katika soko la nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa kuuza bidhaa zao ndani ya nchi wanachama yaani Kenya, Rwanda, Burundi, Uganda pamoja na sisi wenyewe Tanzania .
Wafanyabiashara wanatakiwa kuchangamkia fursa hiyo kwa kuwa ni haki yao na ni utekelezaji wa malengo ya Jumuiya ambayo yemebainishwa katika Mkataba wa uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kifungu namba 5 ambapo Jumuiya ilianzisha Itifaki ya Umoja wa Forodha (The East African Community Customs Union).
Chini ya Itifaki hiyo wafanyabiashara wa Nchi Wanachama wana uhuru wa kufanyabiashara ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki bila kutozwa ushuru wa forodha ilimradi bidhaa zao zimezingatia vigezo na kufuata utaratibu ulioainishwa katika Itifaki hii.
Japokuwa Sudan Kusini imeridhia kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki bado fursa za kufanya biashara nchini humo hazijakamilika. Hii ni kwasababu nchi hiyo imejiunga na Jumuiya hivi karibuni na hadi hapo itakaporejesha ‘Instrument’ yaani zile hati za kujiunga na Jumuiya baada ya kufuata utaratibu wa nchi hiyo, ndipo itakuwa mwanachama kamili ambaye atafurahia matunda haya tunayoyaongelea hapa. Yaani, Sudani Kusini itaingia kwenye utaratibu wa utekelezaji wa Itifaki na makubaliano mbalimbali yaliyofikiwa katika Jumuiya.
Ili mfanyabiashara hasa mdogo aweze kufanya biashara katika Soko la Jumuiya hii anapaswa kufuata utaratibu ufuatao:
a. Mfanyabiashara/ Msafirishaji anatakiwa kufika kwenye kituo chochote cha forodha kilichopo mpakani akiwa na bidhaa yake anayotaka kuuza kwenye Soko la Jumuiya.
b. Akiwa Kituoni hapo, msafirishaji atatakiwa kupatiwa cheti cha Uasilia wa Bidhaa Kilichorahisishwa (Simplified Certificate of Origin) ambacho hutolewa bure na ofisi za Mamlaka ya Forodha Tanzania zilizopo mipakani.
c. Mfanyabiashara atatakiwa kujaza taarifa zinazotakiwa kwenye cheti hicho kama vile jina kamili la msafirishaji, anuani, nchi anayotoka, maelezo ya bidhaa na thamani ya bidhaa. Afisa forodha wa kituo husika atajaza maeneo yanayomhusu na kugonga muhuri katika cheti hicho.
d. Mfanyabiashara atatakiwa kuonesha cheti cha uasilia wa bidhaa wakati akiingia kwenye nchi mwanachama anapotaka kuuza bidhaa hiyo.
e. Cheti cha uasilia wa bidhaa ni kwa ajili ya mfanyabiashara mdogo mwenye bidhaa isiyozidi dola za Kimarekani 2000. Aidha, mfanyabiashara mdogo halazimiki kuwa na wakala wa Forodha.
f. Mfanyabiashara mdogo anatakiwa kufuata taratibu zinazohitajika na taasisi nyingine zinazohusika katika kuruhusu uingizaji / uagizaji wa bidhaa kama vile:
· Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA),
· Shirikia la Viwango Tanzania (TBS) na mamlaka nyingine.
Wizara inatoa wito kwa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla iwapo watakutana na vikwazo visivyo vya kiforodha wakiwa katika Nchi Wanachama, wawasilane na Wizara kupitia Mawasiliano yaliyoanishwa hapo juu.
Aidha, wafanyabiashara pia wanaweza kutoa taarifa za vikwazo wanavyokutana navyo kupitia mfumo wa ujumbe mfupi kwa kuandika neno ‘NTB’ na kutuma kwenda namba 15539. Vilevile kwa madereva wa magari makubwa wanaosafirisha mizigo kwenda Nchi Wanachama utaratibu umewekwa ambapo madereva hao wanaweza kutoa taarifa za moja kwa moja kwa Jeshi la Polisi kupitia namba 0713631780 iwapo watakutana na vikwazo visivyo vya Kiforodha vya barabarani. Kadhalika wafanyabiashara pia wanaweza kuwasilisha malalamiko yao juu ya Vikwazo visivyo vya Kiforodha kupitia tovuti ambayo ni www.tradebarriers.org
Wizara inahimiza wafanyabiashara kutumia njia halali za kuvusha bidhaa kwenye mipaka ya Nchi wanachama kwani njia zisizo halali (Njia za panya) hupelekea wafanyabiashara wengi kudhulumiwa bidhaa au mali zao, kuvamiwa, kuumia na wakati mwingine kuuza bidhaa kwa bei ya hasara. Watanzania wanaweza kufanya biashara ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na bidhaa zao kutolipa ushuru wa forodha ilimradi wamezingatia taratibu zilizokubalika katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Aidha, mfanyabiashara atatakiwa kuwa na hati ya kusafiria pindi anapotaka kuvuka mpaka kwenda Nchi Mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 16 Juni 2016.
Wednesday 15 June 2016
Katibu Mkuu Balozi Dkt. Aziz P. Mlima ( wa nne kutoka kulia waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Liberat Mfumukeko anayefuata kushoto kwake, Makatibu Wakuu kutoka Wizara zinazosimamia masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na wataalam kutoka Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kikao cha Retreaty ya Makatibu Wakuu unaoendelea Mjini Moshi.
Tuesday 14 June 2016
KATIBU MKUU AKIWA KWENYE SHEREHE ZA KUFUNGA MAFUNZO MAALUM YA JKT
Mmoja wa wahitimu wa mafunzo maalum ya JKT akitoa salaam maalum ya kijeshi kwa Kattibu Mkuu Balozi Dkt. Aziz P. Mlima |
Katibu Mkuu Balozi Dkt Aziz P. Mlima akimpongeza mmoja wa wahitimu waliofanya vizuri zaidi wakati wa mafunzo maalum ya JKT |
Katibu Mkuu Balozi Dkt Aziz P. Mlima akikagua gwaride liliondaliwa wakati wa sherehe za kufunga mafunzo maalum ya JKT |
Katibu Mkuu Balozi Dkt. Aziz P. Mlima (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Jeshi mara baada ya kuwasili viunga vya Kikosi namba 832 KJ Ruvu tayari kwa ufunguzi wa sherehe za kufunga mafunzo maalum ya JKT wapili kulia ni Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi Rasrimali watu Bibi Mary Fidelis |
Katibu Mkuu Balozi Dkt Azizi P. Mlima (kushoto) akitembelea mradi wa shamba la migomba la Kikosi namba 832 KJ Ruvu kabla ya kuanza kwa sherehe za kufunga mafunzo maaalum ya JKT, wakawanza kulia Mkuu wa Kikosi hicho Luteni Kanali Charles Mbuge. |
Katibu Mkuu Balozi Dkt Aziz P. Mlima (wakwanza kushoto) akipewa maelezo na Mkuu wa Kikosi namba 832 KJ Ruvu Luteni Kanali Charles Mbuge (wapili kulia) alipotembelea mradi wa kufuga kuku unaosimamiwa na kikosi kabla ya kuanza kwa sherehe za kufunga mafunzo maalum ya JKT (operasheni kikwete) yalifanyika katika viwanja vya JKT Ruvu. Mafunzo haya ya wiki sita (6) yalihusisha watumishi 30 wa Wizara ( 13 kati yao wakiwa ni wasichana na 17 ni Wavulana) |
KATIBU MKUU AKUTANA NA BALOZI WA SWEDEN NCHINI
Katibu Mkuu Balozi Dkt. Aziz P.Mlima na Mhe. Balozi Katarina Rangnit wakijadili jambo kwenye Mkutano uliofanyika Juni 13, 2016, Wizarani, wanaofuatilia kulia ni Wakurugenzi kutoka Wizarani Bw. Geoffrey Mwambe, Bw. Oswald Kyamani na Bw. Eliabi Chodota. |
Katibu Mkuu Balozi Dkt. Aziz P Mlima akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Sweden Nchini Mhe. Balozi Katarina Rangnitt alipomtembelea Wizarani, Juni 13, 2016.
Katibu Mkuu Balozi Dkt. Aziz Mlima na Mhe. Balozi Katarina Rangnitt wakiwasilikiza Mkurugenzi Mkazi wa TMEA Dkt. Josaphat Kweka ( wa kwanza kushoto kwa Balozi), Bi Sara Spant kutoka Ubalozi wa Sweden na Bw. Ulf Ekdahl kutoka Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) katika Mkutano uliofanyika Wizarani Juni 13,2016 |
Subscribe to:
Posts (Atom)