Jumla ya vikwazo visivyo vya
kiushuru (NTBs) nane vilivyoripotiwa vimepatiwa ufumbuzi katika Mkutano wa 15 wa
kikanda uliofanyika Jijini Arusha kuanzia tarehe 25 - 27 Septemba, 2014.
Miongoni mwa vikwazo hivyo nane
vilivotajwa kupatiwa ufumbuzi, vitatu
kutoka Tanzania, kimoja kilihusu Nchi zote Wanachama na vinne Nchi nyingine
wanachama.
Kwa upande wake Tanzania
iliwasilisha taarifa ya kupunguzwa kwa idadi ya vituo vya mizani katika lango
la kati ambavyo kwa sasa vimebaki sita kati ya 15 vya awali.
Hatua hii imechukuliwa sambamba
na kuondolewa kwa vituo vya ukaguzi vya Polisi.
Katika mkutano huo Tanzania
ilitoa taarifa ya kuongezwa kwa magari matano ya polisi kwa lengo la kuimarisha
shughuli za doria katika lango la kati.
Aidha, katika mkutano huo vikwazo
vingine vipya nane vya kibiashara viliripotiwa, kati ya hivyo vikwazo viwili viliripotiwa
na Kenya dhidi ya Uganda, na Uganda dhidi ya Kenya iliripoti
vikwazo vitano,na kikwazo kimoja kiliripotiwa na Tanzania dhidi ya Kenya.
Vikwazo
vilivyoonekana kuleta utata Mkutano uliadhimia vilipelekwe kwenye Baraza la
Mawaziri la Kisekta la Afrika Mashariki la Biashara, Viwanda, Fedha na
Uwekezaji.
Miongoni mwa
vikwazo vilivyotajwa kupelekwa kwenye Baraza la Mawaziri la Kisekta la
Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji ni pamoja na kupima katika mizani magari
matupu ya mizigo, Usajili wa bidhaa
kutoka Mamlaka ya Dawa na Chakula, Mahitaji ya nembo au jina kutoka Mamlaka ya
Dawa na Chakula na mahitaji ya chanjo ya homa ya manjano.
Ilipendekezwa
kuwa vikwazo vinavyolalamikiwa kutoka Mamlaka ya Dawa na Chakula vipelekwe Bodi
ya Viwango ya Afrika Mashariki kwa ajili ya kupata maoni ya kitaalamu
yatakayosaidia kupatikana kwa ufumbuzi.
Kwa Upande
wake Serikali ya Tanzania imedhamiria kupunguza idadi ya vituo vya mizani
kutoka vituo sita vya sasa mpaka vituo vitatu ifikapo June 2015.
Na Teodos
Komba
No comments:
Post a Comment