Wednesday 18 February 2015

MKUTANO WA 16 WA VIONGOZI WAKUU WA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUFANYIKA NAIROBI, KENYA.



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MKUTANO WA 16 WA VIONGOZI WAKUU WA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUFANYIKA NAIROBI, KENYA
Mkutano wa 16 wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki unatarajiwa Kufanyika 20 Februari, 2015 Nairobi, Kenya katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta. Mkutano huu utatanguliwa na Mkutano wa dharura wa  Baraza la Mawaziri la Jumuiya Jumuiya Afrika Mashariki. Pamoja na mambo mengine Mkutano wa Viongozi wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya  Afrika Mashariki unatarajia kufanya yafuatayo;
·         Kupitia taarifa ya Mwaka ya Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kipindi cha Disemba 2013 hadi Novemba 2014,
·         Kupitia taarifa ya utekelezaji wa maamuzi ya Vikao vya Jumuiya ya Afrika     Mashariki
·         Kupitia taarifa ya Masuala ya kiutumishi yakiwemo; uteuzi wa Jaji wa Mahakama ya Rufaa ya Jumuiya Afrika Mashariki, Jaji wa Mahakama ya kwanza ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, uteuzi wa Naibu katibu Mkuu wa Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Jamhuri ya Burundi na kuongeza Muda wa Mkataba wa Naibu katibu Mkuu wa Jumuiya kutoka Jamhuri ya Uganda.
Aidha katika Mkutano huu wa Wakuu wa Nchi wanatarajia kuzindua mpango wa kisasa wa kufanya Mikutano kwa Njia ya Video. (Video Confrence)

Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaotararijiwa kuhudhuria katika Mkutano huu ni Mhe. Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania, Mhe. Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi, Mhe. Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda, Mhe. Rais Paul Kagame wa Rwanda, na  Mhe. Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ambaye ni mwenyeji wa Mkutano.

Imetolewa na;
Katibu Mkuu
WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI


No comments:

Post a Comment