Bunge la Jumuiya ya
Afrika Mashariki (BJAM) leo limeanza vikao vyake Mjini Bujumbura, Burundi. Mkutano
huu wa tano wa Bunge la tatu la Jumuiya ya Afrika Mashariki utafanyika
kwa kipindi cha siku kumi na mbili (12) kuanzia leo Machi 16, 2015 hadi Machi
27, 2015.
Kesho Machi 17,
2015 Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza anatarajiwa kulihutubia
Bunge hilo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki pia
anatarajiwa kulihutubia Bunge hilo(BJAM) Machi 19, 2015.
Bunge hili likiongozwa
na Spika wake Mhe. Daniel F. Kedega katika vikao vyake litajadili Misuada
ifuatayo; Musuada wa marekebisho wa Sheria ya usimamizi wa Umoja wa Forodha ya
Mwaka 2015, Musuada wa marekebisho wa Sheria
ya ushindani ya Mwaka 2015, Musuada wa marekebisho wa Sheria itakayo ruhusu
mawakili kutoa huduma za kisheria ndani ya Nchi Wanachama za Jumuiya ya Afrika
Mashariki ya Mwaka 2014, pamoja na Musuada wa Marekebisho wa Sheria ya Muamala
wa Kielectroniki ya Mwaka 2014.
Pamoja na mambo mengine
Bunge hili la Jumuiya ya Afrika
Mashariki katika Vikao vyake linatarajia kupokea taarifa mbalimbali kutoka kwa Kamati zake. Taarifa
hizo zinahusisha, taarifa kutoka Kamati ya Uhasibu ya ukaguzi ya Juni 30, 2013,
taarifa kutoka Kamati ya Mawasiliano inayohusu Biashara na Uwekezaji katika
eneo la Himaya ya Umoja wa Forodha na taarifa kutoka Kamati ya Malengo ya
Pamoja inayohusu Haki za Watoto wa Nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika
Mashariki.
Aidha, BJAM katika
vikao vyake linatarajia kupitia Kanuni zilizofanyiwa marekebisho na kupitishwa
katika Mkutano wake wa mwisho uliofanyika Januari 2015 Jijini Arusha, Tanzania.
Kwa mujibu wa
ratiba ya Vikao vya Bunge katika Kikao cha nne Mjini Bujumbura litakutana na
Vijana kutoka Burundi na Mabalozi wa Vijana wa Nchi Wanachama za Jumuiya ya
Afrika Mashariki. Katika Kikao hicho wote kwa pamoja wanatarajia kujadili
masuala mbalimbali yanayohusu Jumuiya. Hii ni dhamira ya Bunge la Jumuiya ya Afrika
Mashariki ya kufanya kazi kwa ukaribu na Vijana ambao kwa sasa wanakadiliwa
kuwa ni asilimia 63 ya Idadi ya watu wote wa Afrika Mashariki.
Katika hatua nyingine
Bunge la Jumuiya ya Afrika likiwa Mjini Bujumbura linatarajia kufanya
mazungumzo na wawakilishi wa Wafanyakazi waliopo kwenye Taasisi zilizo chini ya
Shikisho la umoja wa Vyama vya Wafanyakazi wa Afrika Mashariki na wawakilishi
wa Jumuiya ya Waajiri ya Afrika Mashariki.
Wafanyakazi, Vijana, na Waajiri wanatarajiwa kuwasilisha mada zao mbele ya
Bunge ambazo zitatolewa ufumbuzi na Bunge hilo.
Katika kikao cha
Mwisho cha BJAM kilichofanyika Januari 2015
Mjini Arusha, Bunge hilo lilipitisha Misuada miwili, maazimio matatu, na
taarifa nne muhimu. Pia Misuada mingine sita ilisomwa kabla ya kukabidhiwa kwa
Kamati husika.
No comments:
Post a Comment