WIZARA YA MAMBO YA NJE, USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI, KIKANDA NA KIMATAIFA
TAARIFA MUHIMU KWA UMMA
Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki imetangaza nafasi kumi (10) za kazi kupitia mtandao wake www.eac.int tarehe 19/02/2016. Kati ya nafasi hizo, nafasi tano (5) ni za kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki na nafasi tano (5) ni kutoka Tume ya Ushindani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (The EAC Competition Authority).
Maombi ya kazi hizo yanatakiwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambapo tarehe ya mwisho kuwasilisha maombi hayo kwa nafasi za Registrar, Deputy Registrar, Mergers and Acquisitions,Deputy Registrar, Monopolies and Cartels, Accounts Assistant na Senior Personal Secretary ni tarehe 13/03/2016. Kazi hizi ni za mkataba kwa kipindi cha miaka mitano (5) na kurudiwa mara moja kwa kipindi kingine cha miaka mitano kutegemea utendaji kazi wa mtumishi husika. Aidha tarehe ya mwisho ya kuwasilishwa maombi ya na nafasi za Accounts Assistant,Principal Research Fellow,Research Assistant, Senior Research Fellow na EAC Quality Management System (QMS) Focal Officer ni tarehe 18/03/2016. Nafasi hizi za mkataba kwa muda wa mwaka mmoja (1) na utarudiwa kutokana na utendaji kazi wa mtumishi pamoja na upatikanaji wa fedha.
Kwa maelekezo zaidi kuhusu utaratibu wa kuomba, kuwasilisha maombi na maelezo ya ziada tafadhali tembelea tovuti ya Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki : www.eac.int. au kupitia link; bofya hapa
Wizara inapenda kuwaarifu na kuwahamasisha Watanzania wenye sifa stahiki waweze kuomba kazi hizi ili kuongeza ushiriki na uwakilishi wa Tanzania katika Ajira za Jumuiya na hivyo kushiriki ipasavyo katika maamuzi mbalimbali yanayohusu nchi yetu katika Jumuiya.
Watanzania watakaopenda kuwasilisha maombi ya kazi hizo wawasiliane na Wizara hii kupitia Idara ya Utawala kwa maelekezo zaidi kabla hawajatuma maombi yao.
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa
Februari 24, 2016.
No comments:
Post a Comment