Monday, 19 January 2015

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Bw. Amantius C. Msole akiwa katika Mkutano wa kuwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara kwa Kipindi cha Julai – Desemba, 2014 kwa Kamati ya Bunge kwenye Mkutano uliofanyika katika Ofisi ndogo za Bunge Jijini Dsm
Waziri Mh. Samuel Sitta (kulia) akisikiliza maoni ya mjumbe (hayumo pichani) wakati wa uwasilishwaji wa Taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara kwa kipindi cha Julai – Desemba, 2014 kwa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa 16/1/2015.

Waziri Mh. Samuel Sitta (kulia) akiwa na Naibu Waziri Mh. Dk. Abdulla .J. Saadalla (Kushoto) wakati akisisitiza jambo kwenye Mkutano wa kuwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara kwa kipindi cha Julai - Disemba, 2014 kwa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika Ofisi ndogo za Bunge zilizopo Jijini Dar-es-Salaam Tarehe 16/1/2015

Waziri Mh. Samuel Sitta (kulia) akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara kwa kipindi cha Julai – Desemba, 2014 kwa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Tarehe 16/1/2015.

Thursday, 15 January 2015

Wajumbe kutoka Kenya wakiwa katika picha ya pamoja na Wataalam wa Wizara mara baada ya Mkutano wakujadili Masuala mbalimbali yanayohusu Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa upande wa Tanzania na Kenya uliofanyika Hotel ya Ledger Jijini Dsm Tarehe 14/1/2015.

Saturday, 10 January 2015

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar Bw. Said A.S Natepe akisaini Kitabu cha Wageni alipotembelea Banda la Wizara kwenye Tamasha la Pili la Biashara Zanzibar lililofanyika katika Uwanja wa Maisara Mjini Unguja Tarehe 5- 12/1/2015.

Baadhi ya Wananchi waliotembelea Banda la Wizara kwenye Tamasha la Pili la Biashara Zanzibar wakisaini Kitabu cha Wageni. Tarehe 9/1/2015
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Wizara Bi. Robi Bwiru na Maofisa wengine wa Wizara wakitoa Elimu kwa Wananchi waliotembelea Banda la Wizara kwenye Tamasha la Pili la Bishara Zanzibar Tarehe 9/10/2015. 

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji Dr. Abdullah Makame (Kulia) akiwa kwenye Sherehe za Ufunguzi wa Tamasha la Pili la Bishara Zanzibar Kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara Tarehe 9/1/2015.

Mgeni Rasmi, Makamu wa Pili wa Raisi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  Balozi Seif Ali Idd (kulia) akipewa maelezo na Maofisa wa Wizara (hawapo pichani) alipotembelea Banda la Wizara mara baada ya Sherehe za Ufunguzi wa Tamasha la Pili la Biashara Zanzibar.

Monday, 15 December 2014

Mh. Waziri Samuel Sitta (katikati) akipongezwa na Katibu Mkuu Bi. Joyce Mapunjo (kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Raslimali Watu Bi. Vedastina Justinian (kulia) baada ya kutunukiwa Nishani ya Daraja la pili ya Muungano na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sherehe za Uhuru zilizofanyika Viwanja vya Ikulu Jijini Dar-es-Salaam 9/12/2014.

Mh. Waziri Samuel Sitta akiwa katika Picha ya pamoja  na Mh. Rais Dk. Mrisho Jakaya Kikwete baada ya kutunukiwa Nishani ya Daraja la Pili ya Muungano wengine ni Viongozi wa Serikali, Viongozi Wastaafu, na Wengine waliotunukiwa Nishani hiyo katika Sherehe ya Uhuru iliyofanyika Ikulu Jijini Dar-es-Salaam 9/12/2014.

Thursday, 27 November 2014

Naibu Waziri Mh. Dkt. Abdullah Juma Saadalla (Katikati), Katibu Mkuu Bi. Joyce Mapunjo (kushoto) na Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Mh. Nassor Ahmed Mazrui wakiongoza kikao cha majadiliano ya Nchi (Tanzania) leo Nov. 27,2014 jijini Nairobi, Kenya.

Baadhi ya Wajumbe kutoka Tanzania wakiwa katika kikao cha Majadiliano ya ndani kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki Kesho Tarehe 28 Novemba, 2014 Jijini Nairobi, Kenya.

Tuesday, 21 October 2014

Naibu Waziri Dkt. Abdulla Juma Abdulla Saadala  mwenye kofia akioneshwa  namna Meli ya RV Jumuiya ya Ziwa Victoria Jijini Mwanza inavyofanya kazi, ikiwa katika mwendo ndani ya maji na nahodha wa meli hiyo  Captain Juma Nkwama Tarehe 14/10/2014.

Nahodha wa Meli ya RV Jumuiya Capt. Juma Nkwama akionesha furaha yake mara baada ya kumuonesha Naibu Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Abdulla Juma Abdulla Saadala namna Meli hiyo inavyofanyakazi ikiwa ndani ya maji Tarehe 14/10/2014.

Naibu Waziri wa Wizara  ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Abdulla Juma Abdulla Saadala akitiasaini kitabu cha mahudhurio ndani ya Meli ya RV Jumuiya katika Ziwa Victoria Jijini Mwanza Tarehe 14/10/2014.

Naibu Waziri, Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Abdulla Juma Abdulla Saadala akiendesha kikao ndani ya Meli ya RV Jumuiya ya Ziwa Victoria Jijini Mwanza Tarehe 14/10/2014.

Naibu Waziri Dkt. Abdulla Juma Abdulla Saadala akifafanua jambo ndani ya Meli ya RV Jumuiya ya Ziwa Victoria Jijini Mwanza katika kikao chake na nahodha wa Meli hiyo Peter Nkwama na Mhandisi wa meli hiyo Herman Bundala. Tarehe 14/10/2014.

Picha ya Meli ya RV Jumuiya, Meli ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Ziwa Victoria Jijini Mwanza.Tarehe 14/10/2014.

Thursday, 2 October 2014

VIKWAZO NANE VYA KIBIASHARA VYAPATIWA UFUMBUZI

Jumla ya vikwazo visivyo vya kiushuru (NTBs) nane vilivyoripotiwa vimepatiwa ufumbuzi katika Mkutano wa 15 wa kikanda uliofanyika Jijini Arusha kuanzia tarehe 25 - 27 Septemba, 2014.

Miongoni mwa vikwazo hivyo nane vilivotajwa kupatiwa ufumbuzi, vitatu kutoka Tanzania, kimoja kilihusu Nchi zote Wanachama na vinne Nchi nyingine wanachama.

Kwa upande wake Tanzania iliwasilisha taarifa ya kupunguzwa kwa idadi ya vituo vya mizani katika lango la kati ambavyo kwa sasa vimebaki sita kati ya 15 vya awali.

Hatua hii imechukuliwa sambamba na kuondolewa kwa vituo vya ukaguzi vya Polisi.

Katika mkutano huo Tanzania ilitoa taarifa ya kuongezwa kwa magari matano ya polisi kwa lengo la kuimarisha shughuli za doria katika lango la kati.

Aidha, katika mkutano huo vikwazo vingine vipya nane vya kibiashara viliripotiwa, kati ya hivyo vikwazo viwili viliripotiwa na Kenya dhidi ya Uganda, na Uganda dhidi ya Kenya iliripoti vikwazo vitano,na kikwazo kimoja kiliripotiwa na Tanzania dhidi ya Kenya.

Vikwazo vilivyoonekana kuleta utata Mkutano uliadhimia vilipelekwe kwenye Baraza la Mawaziri la Kisekta la Afrika Mashariki la Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji.

Miongoni mwa vikwazo vilivyotajwa kupelekwa kwenye Baraza la Mawaziri la Kisekta la Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji ni pamoja na kupima katika mizani magari matupu ya mizigo, Usajili wa bidhaa kutoka Mamlaka ya Dawa na Chakula, Mahitaji ya nembo au jina kutoka Mamlaka ya Dawa na Chakula na mahitaji ya chanjo ya homa ya manjano. 

Ilipendekezwa kuwa vikwazo vinavyolalamikiwa kutoka Mamlaka ya Dawa na Chakula vipelekwe Bodi ya Viwango ya Afrika Mashariki kwa ajili ya kupata maoni ya kitaalamu yatakayosaidia kupatikana kwa ufumbuzi.

Kwa Upande wake Serikali ya Tanzania imedhamiria kupunguza idadi ya vituo vya mizani kutoka vituo sita vya sasa mpaka vituo vitatu ifikapo June 2015.

Na Teodos Komba