Friday, 22 January 2016

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE, USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI, KIKANDA NA KIMATAIFA
                                                              
Description: Description: Coat of Arms
                         

Simu ya maandishi: ‘MEAC’
Simu Na. 022-2126827, 2126830, 2126823
Fax: 022 – 2126651/2120488
Barua Pepe: ps@meac.go.tz
Tovuti: www.meac.go.tz

NSSF Waterfront Ghorofa ya 5
35 Barabara ya Edward Sokoine
S.L.P 9280,
11467 DAR ES SALAAM,
Tanzania.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MKUTANO WA NNE WA BUNGE LA TATU LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUANZA JIJINI ARUSHA

Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki linatarajia kuanza mkutano wake Jijini Arusha, Tanzania. Mkutano huu wanne wa Bunge la tatu la Jumuiya ya Afrika Mashariki (BJAM) utafanyika kwa siku kumi na mbili (12) kuanzia leo Jumatatu Januari 24, 2016 hadi Ijumaa Februari 5, 2016. 

BJAM ambalo litaongozwa na spika wake Mhe. Daniel F. Kidega, katika vikao vyake litajadili taarifa kutoka kamati mbalimbali zenye mapendekezo kuhusu hatua mbalimbali za mtangamano kutoka kwa wadau sambamba na kujadili taarifa za kamati zifuatazo; 

· Taarifa ya Kamati ya Malengo ya Pamoja inayozungumzia kuhusu maombi ya vibali vya kazi na uraia, kufuatia mapendekezo ya Shirikisho la Wafanyakazi la Afrika Mashariki na Chama cha Waajiri Afrika Mashariki. 

· Kupokea na kujadili taarifa kutoka Kamati ya Sheria na Kinga kuhusu mapendekezo ya maboresho na marekebisho ya kanuni mbalimbali za BJAM. 

Katika hatua nyingine wakati wa Mkutano huu wa Bunge kutakuwa na zoezi la kuapishwa kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Dkt. Suzan Kolimba ili aweze kushiriki katika Vikao vya Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki. 

Aidha, BJAM linatarajia kupokea na kujadili Musuada wa kupunguza majanga ya mwaka 2013 (Disaster Risk Reduction Bill 2013). 

Vilevile, suala la mgogoro wa kisiasa wa Nchini Burundi unatarajiwa kuwa sehemu ya mjadala katika Mkutano huu wa nne wa Bunge hilo. Kamati ya Bunge ya Masuala ya Kikanda na Usuluhishi wa migogoro itamalizia na kuwasilisha taarifa iliyoipokea kutoka Chama cha Wanasheria cha Umoja wa Afrika inayohusu hali ya kisiasa Nchini Burundi. 

Katika BJAM Tanzania inawakilishwa na Wabunge Tisa; Mhe. Charles Makongoro Nyerere ambaye ni Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki, Mhe. Issa Twaha Taslima ambaye ni Katibu, wengine ni Mhe. Abdullah Ally Hassan Mwinyi, Mhe. Shy-Rose Sadrudin Bhanji, Mhe. Adam Omar Kimbisa, Mhe. Angela Charles Kizigha, Mhe. Bernard Musomi Murunya, Mhe.Perpetua Kessy Nderakindo na Mhe. Maryam Ussi Yahya 

Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki linafanya Mikutano yake kwa utaratibu wa Mzunguko miongoni mwa Nchi wanachama kama ilivyoainishwa kwenye Ibara ya 55 ya Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Aidha BJAM linakutana kwa Mwaka mara moja katika Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Arusha, Tanzania. 

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Mambo ya Nje,Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa
Dar es Salaam, Januari 23, 2016

Tuesday, 19 January 2016

Tanzania: Tupo tayari kushiriki katika Mazungumzo ya Burundi


Tanzania: Tupo tayari kushiriki katika Mazungumzo ya Burundi.

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Maiga akizumgumza na waandishi wa habari mwishoni wa wiki alisema Tanzania ipo tayari kushiriki katika mazungumzo ya kuiletea amani Burundi kadri itakavyo amliwa na Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki unaotarajiwa kufanyika siku za karibuni.

Katika Mkutano huo na waandishi wa habari ambao pia alishiriki Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi Mhe. Alain Aime Nyamitwe, Waziri Mhe. Balozi Dkt Maiga ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki alisema “nimempokea Waziri wa Burundi leo, sababu ya ujio wake ni kutoa ishara na uthibitisho kuwa Burundi iko tayari kutushirikisha katika kutafuta suluhu na amani tukiwa kama wenyekiti, ni jambo la kufurahisha pia kuona mazungumzo ya amani yanaendelea baina ya Warundi wenyewe, na kwa kuhusisha Mataifa mengine katika kuleta amani”. 

Aidha kwa upande wake Waziri wa mambo Mambo ya Nje wa Nchini Burundi Mhe.Alain Aime Nyamitwe katika Mkutano huo alisema Burundi ikotayari kuendelea na mazungumzo ya kuleta amani nchini humo kufuatia changamoto za kiusalama zinazo ikabili Nchi hiyo baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika Julai 21, 2015.

“Hali ya Burundi ni salama, tunakabiliwa na changamoto chache za kiusalama katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Bujumbura lakini ukienda maeneo ya vijijini hali ni shwari kabisa na wananchi wanaendelea na kazi zao za kila siku kama kawaida na Serikali inajitahidi kufanya kila linalowezeakana kuhakikisha changamo hizi za kiusalama zinatatuliwa mapema iwezekanavyo” alisema Mhe. Nyamitwe. 

Aliongeza kusema Mazungumzo ya ndani ya Nchi na Msuluhishi yanaendelea pia kwa kuhushikisha makundi mbalimbali ya kijamii zikiwemo asasi za kiraia, viongozi wa dini na wananchi wote kwa ujumla.


Mhe. Nyamitwe aliwasili Jijini Dar es Salaam Ijumaa tarehe 15/01/2016 kumtembelea Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Maiga ambapo baada ya mazungumzo kwa pamoja waliongea na vyombo vya habari katika Mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi mdogo wa Mikutano wa Wizara. Kwa wakati huu Tanzania ni Mwenyeki wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

WIZARA YAFANYA KIKAO NA WABUNGE WA AFRIKA MASHARIKI

Mhe. Waziri Balozi Dkt. Augustine Mahiga (wakwanza kulia), akizungumza na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki wa Tanzania wakati wa kikao kati ya Wizara na Wabunge hao.




(Kulia-kushoto) Ni Mhe. Waziri Balozi Dkt. Augustine Mahiga, Naibu Waziri Mhe. Dkt. Suzan Kolimba, wakibadilishana mawazo na Waheshimiwa Wabunge wa Afrika Mashariki, Mhe. Charles Makongoro Nyerere, Mhe. Shy-Rose Sadrudin Bhanji, Mhe. Angel Charlers Kizigha na Mhe. Bernard Musomi Murunya. 


Monday, 18 January 2016


Mhe. Waziri Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) na Mhe. Naibu Waziri Dkt. Suzan Kolimba (kushoto-walioketi) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki na baadhi ya watendaji wa Wizara.

Saturday, 16 January 2016

HABARI KATIKA PICHA

Waziri wa Mambo ya Nje wa Nchini Burundi Mhe. Alain Aime Nyamitwe (kushoto) akifanunua jambo kwa waandishi wa habari wakati akizungumza na waandishi hao Jijini Dar es Salaam, Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Maiga.
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Maiga (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)  katika ukumbi mdogo wa mikutano wa  Wizara, Jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Nchini Burundi Mhe. Alain Aime Nyamitwe 15/01/2016.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Nchini Burundi Mhe. Alain Aime Nyamitwe (kushoto) akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) alipomtembelea Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa wa Nchini Tanzania Mhe. Balozi Augustine Maiga (katikati), kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasilino  Serikalini  Wizara ya Mambo Nje Bi. Mindi Kasiga 15/01/2016,
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Maiga (kulia) akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Nchini Burundi Mhe. Alain Aime Nyamitwe (kushoto) alipomtembea Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam 15/01/2016. 
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Maiga (kulia) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Nchini Burundi Mhe. Alain Aime Nyamitwe (kushoto) alipomtembea Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam 15/01/2016.







Wednesday, 30 December 2015

MAONESHO YA 16 YA JUAKALI/NGUVUKAZI YALIYOFANYIKA MNAZIMMOJA DAR, NOVEMBER30 - DICEMBER 6, 2015

Katibu Mkuu Bibi Joyce Mapunjo akiongea na wajasiriamali wakati wa maonesho ya Juakali/Nguvukazi 
Mjasiriamali anayezalisha bidhaa za ngozi kutoka Nchini Rwanda (kulia) akitoa maelezo ya bidhaa zake kwa Afisa sheria Bw. Beatus Kalumuna (kushoto) katika maonesho ya 16 ya Juakali/Nguvukazi yaliyofanyika viwanja vya mnazimmoja Jijini Dar 4/12/2015.
Katibu Mkuu Bibi Joyce Mapunjo akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Banda la Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenye maonesho ya 16 ya Juakali/Nguvukazi yaliyofanyika viwanja vya Mnazimmoja Jijini Dar 2/12/2015
Mkurugenzi Msaidizi wa Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji Bw. Bernard Haule (kulia) Mkurugenzi Msaidizi wa Siasa, Ulinzi, na Usalama Bw. Amani Mwatonoka (kushoto) wakipewa maelezo kutoka kwa Afisa Biashara wa Wizara Bibi Vivian Rutaihwa walipotembelea banda la Tanzania kwenye maonesho ya 16 ya Juakali/Nguvukazi yaliyofanyika viwanja vya mnazimmoja Jijini Dar 1/012/2015.
Wajasiriamali wakiwa katika banda la maonesho ya bidhaa katika maonesho ya 16 ya Juakali/Nguvukazi yaliyofanyika mnazimmo jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 30 Novemba hadi 6 Disemba 2015
Wajasiriamali wakiwa katika banda la maonesho ya bidhaa katika maonesho ya 16 ya Juakali/Nguvukazi yaliyofanyika mnazimmo jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 30 Novemba hadi 6 Disemba 2015
Bidhaa mbalimbali za wajasiriamali zikiwa kwenye mabanda ya maonesho ya Juakali/Nguvukazi yaliyofanyika kwenye uwanja wa Mnazimmoja Jijini Dar es Salaam.
Wajasiriamali wakiwa katika banda la maonesho ya bidhaa katika maonesho ya 16 ya Juakali/Nguvukazi yaliyofanyika mnazimmo jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 30 Novemba hadi 6 Disemba 2015.
Wananchi wakiangalia mashine ya kusaga vyakula vya mifugo na nafaka iliyobuniwa na mjasiriamali katika maonesho ya 16 ya Juakali/Nguvukazi yaliyofanyika viwanja vya Mnazimmoja jijini Dar 2/12/2015.