Monday, 19 January 2015
Thursday, 15 January 2015
Saturday, 10 January 2015
![]() |
| Baadhi ya Wananchi waliotembelea Banda la Wizara kwenye Tamasha la Pili la Biashara Zanzibar wakisaini Kitabu cha Wageni. Tarehe 9/1/2015 |
Monday, 15 December 2014
Mh. Waziri Samuel Sitta (katikati) akipongezwa na Katibu Mkuu Bi. Joyce Mapunjo (kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Raslimali Watu Bi. Vedastina Justinian (kulia) baada ya kutunukiwa Nishani ya Daraja la pili ya Muungano na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sherehe za Uhuru zilizofanyika Viwanja vya Ikulu Jijini Dar-es-Salaam 9/12/2014.
Mh. Waziri Samuel Sitta (katikati) akipongezwa na Katibu Mkuu Bi. Joyce Mapunjo (kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Raslimali Watu Bi. Vedastina Justinian (kulia) baada ya kutunukiwa Nishani ya Daraja la pili ya Muungano na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sherehe za Uhuru zilizofanyika Viwanja vya Ikulu Jijini Dar-es-Salaam 9/12/2014.
Thursday, 27 November 2014
Baadhi ya Wajumbe kutoka Tanzania wakiwa katika kikao cha Majadiliano ya ndani kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki Kesho Tarehe 28 Novemba, 2014 Jijini Nairobi, Kenya.
Baadhi ya Wajumbe kutoka Tanzania wakiwa katika kikao cha Majadiliano ya ndani kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki Kesho Tarehe 28 Novemba, 2014 Jijini Nairobi, Kenya.
Tuesday, 21 October 2014
Naibu Waziri Dkt. Abdulla Juma Abdulla Saadala
mwenye kofia akioneshwa namna Meli
ya RV Jumuiya ya Ziwa Victoria Jijini Mwanza inavyofanya kazi, ikiwa katika
mwendo ndani ya maji na nahodha wa meli hiyo Captain Juma Nkwama Tarehe
14/10/2014.
Nahodha wa Meli ya RV Jumuiya Capt. Juma Nkwama
akionesha furaha yake mara baada ya kumuonesha Naibu Waziri wa Wizara ya
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Abdulla Juma Abdulla Saadala namna Meli
hiyo inavyofanyakazi ikiwa ndani ya maji Tarehe 14/10/2014.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Abdulla Juma
Abdulla Saadala akitiasaini kitabu cha mahudhurio ndani ya Meli ya RV Jumuiya
katika Ziwa Victoria Jijini Mwanza Tarehe 14/10/2014.
Naibu Waziri, Wizara ya Ushirikiano
wa Afrika Mashariki Dkt. Abdulla Juma Abdulla Saadala akiendesha kikao ndani ya
Meli ya RV Jumuiya ya Ziwa Victoria Jijini Mwanza Tarehe 14/10/2014.
Naibu Waziri Dkt. Abdulla Juma Abdulla
Saadala akifafanua jambo ndani ya Meli ya RV Jumuiya ya Ziwa Victoria Jijini
Mwanza katika kikao chake na nahodha wa Meli hiyo Peter Nkwama na Mhandisi wa
meli hiyo Herman Bundala. Tarehe 14/10/2014.
Picha ya Meli ya RV Jumuiya, Meli ya Jumuiya ya
Afrika Mashariki ya Ziwa Victoria Jijini Mwanza.Tarehe 14/10/2014.
Thursday, 2 October 2014
VIKWAZO NANE VYA KIBIASHARA VYAPATIWA UFUMBUZI
Jumla ya vikwazo visivyo vya
kiushuru (NTBs) nane vilivyoripotiwa vimepatiwa ufumbuzi katika Mkutano wa 15 wa
kikanda uliofanyika Jijini Arusha kuanzia tarehe 25 - 27 Septemba, 2014.
Miongoni mwa vikwazo hivyo nane
vilivotajwa kupatiwa ufumbuzi, vitatu
kutoka Tanzania, kimoja kilihusu Nchi zote Wanachama na vinne Nchi nyingine
wanachama.
Kwa upande wake Tanzania
iliwasilisha taarifa ya kupunguzwa kwa idadi ya vituo vya mizani katika lango
la kati ambavyo kwa sasa vimebaki sita kati ya 15 vya awali.
Hatua hii imechukuliwa sambamba
na kuondolewa kwa vituo vya ukaguzi vya Polisi.
Katika mkutano huo Tanzania
ilitoa taarifa ya kuongezwa kwa magari matano ya polisi kwa lengo la kuimarisha
shughuli za doria katika lango la kati.
Aidha, katika mkutano huo vikwazo
vingine vipya nane vya kibiashara viliripotiwa, kati ya hivyo vikwazo viwili viliripotiwa
na Kenya dhidi ya Uganda, na Uganda dhidi ya Kenya iliripoti
vikwazo vitano,na kikwazo kimoja kiliripotiwa na Tanzania dhidi ya Kenya.
Vikwazo
vilivyoonekana kuleta utata Mkutano uliadhimia vilipelekwe kwenye Baraza la
Mawaziri la Kisekta la Afrika Mashariki la Biashara, Viwanda, Fedha na
Uwekezaji.
Miongoni mwa
vikwazo vilivyotajwa kupelekwa kwenye Baraza la Mawaziri la Kisekta la
Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji ni pamoja na kupima katika mizani magari
matupu ya mizigo, Usajili wa bidhaa
kutoka Mamlaka ya Dawa na Chakula, Mahitaji ya nembo au jina kutoka Mamlaka ya
Dawa na Chakula na mahitaji ya chanjo ya homa ya manjano.
Ilipendekezwa
kuwa vikwazo vinavyolalamikiwa kutoka Mamlaka ya Dawa na Chakula vipelekwe Bodi
ya Viwango ya Afrika Mashariki kwa ajili ya kupata maoni ya kitaalamu
yatakayosaidia kupatikana kwa ufumbuzi.
Kwa Upande
wake Serikali ya Tanzania imedhamiria kupunguza idadi ya vituo vya mizani
kutoka vituo sita vya sasa mpaka vituo vitatu ifikapo June 2015.
Na Teodos
Komba
Subscribe to:
Posts (Atom)

























