Monday 5 October 2015

                       

                      JAMHURI YA MUUNGANO WA                            TANZANIA
WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


  MKUTANO WA PILI WA BUNGE LA JUMUIYA YA  AFRIKA MASHARIKI KUANZA                                                                                   LEO.

Mkutano wa pili, kipindi cha nne wa Bunge la tatu la Jumuiya ya Afrika Mashariki unaanza leo tarehe 5 Oktoba, 2015 Jijini Nairobi, Nchini Kenya, ukumbi wa Bunge la Nchi hiyo. Mkutano huu unatarajiwa kufanyika kwa siku 11, kuanzia tarehe 5 hadi 15 Oktoba 2015.

Mkutano huu unatarajiwa kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta siku ya jumanne tarehe 6 Oktoba, 2015.

Katika Mkutano huu, Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (BJAM) pamoja na mambo mengine litatumia vikao vyake kupokea na kujadili ripoti za kamati mbalimbali za Bunge na kujadili miswada mitatu ya kisheria. Miswada hiyo itakayo jadiliwa ni;

· Muswada wa sheria wa miamala ya elektoniki wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa mwaka 2014 (The EAC Electronic Transaction Bill 2014).

· Muswada wa Sheria ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wa kusimamia na kulinda Misitu wa Mwaka 2015 (The EAC Forests Management and Protection Bill 2015).

· Muswada wa Sheria ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wa kupunguza na kukabiliana na majanga (The East African Community Disaster Risk Reduction and Management Bill)

Katika Mkutano huu wa pili wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kulihutubia Bunge hilo tarehe 12 Octoba, 2015 na atatumia fursa hii kuliaga Bunge hilo.

                     
                                                 Imetolewa na,
                      Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.



No comments:

Post a Comment