Monday, 15 December 2014


Mh. Waziri Samuel Sitta (katikati) akipongezwa na Katibu Mkuu Bi. Joyce Mapunjo (kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Raslimali Watu Bi. Vedastina Justinian (kulia) baada ya kutunukiwa Nishani ya Daraja la pili ya Muungano na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sherehe za Uhuru zilizofanyika Viwanja vya Ikulu Jijini Dar-es-Salaam 9/12/2014.








Mh. Waziri Samuel Sitta (katikati) akipongezwa na Katibu Mkuu Bi. Joyce Mapunjo (kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Raslimali Watu Bi. Vedastina Justinian (kulia) baada ya kutunukiwa Nishani ya Daraja la pili ya Muungano na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sherehe za Uhuru zilizofanyika Viwanja vya Ikulu Jijini Dar-es-Salaam 9/12/2014.




Mh. Waziri Samuel Sitta akiwa katika Picha ya pamoja  na Mh. Rais Dk. Mrisho Jakaya Kikwete baada ya kutunukiwa Nishani ya Daraja la Pili ya Muungano wengine ni Viongozi wa Serikali, Viongozi Wastaafu, na Wengine waliotunukiwa Nishani hiyo katika Sherehe ya Uhuru iliyofanyika Ikulu Jijini Dar-es-Salaam 9/12/2014.

Thursday, 27 November 2014




Naibu Waziri Mh. Dkt. Abdullah Juma Saadalla (Katikati), Katibu Mkuu Bi. Joyce Mapunjo (kushoto) na Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Mh. Nassor Ahmed Mazrui wakiongoza kikao cha majadiliano ya Nchi (Tanzania) leo Nov. 27,2014 jijini Nairobi, Kenya.

Naibu Waziri Mh. Dkt. Abdullah Juma Saadalla (Katikati), Katibu Mkuu Bi. Joyce Mapunjo (kushoto) na Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Mh. Nassor Ahmed Mazrui wakiongoza kikao cha majadiliano ya Nchi (Tanzania) leo Nov. 27,2014 jijini Nairobi, Kenya.


 Naibu Waziri Mh. Dkt. Abdullah Juma Saadalla (Katikati), Katibu Mkuu Bi. Joyce Mapunjo (kushoto) na Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Mh. Nassor Ahmed Mazrui wakiongoza kikao cha majadiliano ya Nchi (Tanzania) leo Nov. 27,2014 jijini Nairobi, Kenya.


Baadhi ya Wajumbe kutoka Tanzania wakiwa katika kikao cha Majadiliano ya ndani kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki Kesho Tarehe 28 Novemba, 2014 Jijini Nairobi, Kenya.


Baadhi ya Wajumbe kutoka Tanzania wakiwa katika kikao cha Majadiliano ya ndani kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki Kesho Tarehe 28 Novemba, 2014 Jijini Nairobi, Kenya.


 Baadhi ya Wajumbe kutoka Tanzania wakiwa katika kikao cha Majadiliano ya ndani kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki Kesho Tarehe 28 Novemba, 2014 Jijini Nairobi, Kenya.

 Baadhi ya Wajumbe kutoka Tanzania wakiwa katika kikao cha Majadiliano ya ndani kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki Kesho Tarehe 28 Novemba, 2014 Jijini Nairobi, Kenya.

Tuesday, 21 October 2014





Naibu Waziri Dkt. Abdulla Juma Abdulla Saadala  mwenye kofia akioneshwa  namna Meli ya RV Jumuiya ya Ziwa Victoria Jijini Mwanza inavyofanya kazi, ikiwa katika mwendo ndani ya maji na nahodha wa meli hiyo  Captain Juma Nkwama Tarehe 14/10/2014.




Nahodha wa Meli ya RV Jumuiya Capt. Juma Nkwama akionesha furaha yake mara baada ya kumuonesha Naibu Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Abdulla Juma Abdulla Saadala namna Meli hiyo inavyofanyakazi ikiwa ndani ya maji Tarehe 14/10/2014.




Naibu Waziri wa Wizara  ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Abdulla Juma Abdulla Saadala akitiasaini kitabu cha mahudhurio ndani ya Meli ya RV Jumuiya katika Ziwa Victoria Jijini Mwanza Tarehe 14/10/2014.




Naibu Waziri, Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Abdulla Juma Abdulla Saadala akiendesha kikao ndani ya Meli ya RV Jumuiya ya Ziwa Victoria Jijini Mwanza Tarehe 14/10/2014.



Naibu Waziri Dkt. Abdulla Juma Abdulla Saadala akifafanua jambo ndani ya Meli ya RV Jumuiya ya Ziwa Victoria Jijini Mwanza katika kikao chake na nahodha wa Meli hiyo Peter Nkwama na Mhandisi wa meli hiyo Herman Bundala. Tarehe 14/10/2014.





Picha ya Meli ya RV Jumuiya, Meli ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Ziwa Victoria Jijini Mwanza.Tarehe 14/10/2014.








                                                                




Thursday, 2 October 2014

VIKWAZO NANE VYA KIBIASHARA VYAPATIWA UFUMBUZI




Jumla ya vikwazo visivyo vya kiushuru (NTBs) nane vilivyoripotiwa vimepatiwa ufumbuzi katika Mkutano wa 15 wa kikanda uliofanyika Jijini Arusha kuanzia tarehe 25 - 27 Septemba, 2014.

Miongoni mwa vikwazo hivyo nane vilivotajwa kupatiwa ufumbuzi, vitatu kutoka Tanzania, kimoja kilihusu Nchi zote Wanachama na vinne Nchi nyingine wanachama.

Kwa upande wake Tanzania iliwasilisha taarifa ya kupunguzwa kwa idadi ya vituo vya mizani katika lango la kati ambavyo kwa sasa vimebaki sita kati ya 15 vya awali.

Hatua hii imechukuliwa sambamba na kuondolewa kwa vituo vya ukaguzi vya Polisi.

Katika mkutano huo Tanzania ilitoa taarifa ya kuongezwa kwa magari matano ya polisi kwa lengo la kuimarisha shughuli za doria katika lango la kati.

Aidha, katika mkutano huo vikwazo vingine vipya nane vya kibiashara viliripotiwa, kati ya hivyo vikwazo viwili viliripotiwa na Kenya dhidi ya Uganda, na Uganda dhidi ya Kenya iliripoti vikwazo vitano,na kikwazo kimoja kiliripotiwa na Tanzania dhidi ya Kenya.

Vikwazo vilivyoonekana kuleta utata Mkutano uliadhimia vilipelekwe kwenye Baraza la Mawaziri la Kisekta la Afrika Mashariki la Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji.

Miongoni mwa vikwazo vilivyotajwa kupelekwa kwenye Baraza la Mawaziri la Kisekta la Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji ni pamoja na kupima katika mizani magari matupu ya mizigo, Usajili wa bidhaa kutoka Mamlaka ya Dawa na Chakula, Mahitaji ya nembo au jina kutoka Mamlaka ya Dawa na Chakula na mahitaji ya chanjo ya homa ya manjano. 

Ilipendekezwa kuwa vikwazo vinavyolalamikiwa kutoka Mamlaka ya Dawa na Chakula vipelekwe Bodi ya Viwango ya Afrika Mashariki kwa ajili ya kupata maoni ya kitaalamu yatakayosaidia kupatikana kwa ufumbuzi.

Kwa Upande wake Serikali ya Tanzania imedhamiria kupunguza idadi ya vituo vya mizani kutoka vituo sita vya sasa mpaka vituo vitatu ifikapo June 2015.

Na Teodos Komba

Friday, 12 September 2014

Mara Milele: Zaidi ya watu 300,000 wanatarajiwa kuhudhuria maadhimisho ya siku ya Mara (Mara Day Celebrations)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Zaidi ya watu 300,000 wanatarajiwa kuhudhuria Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Mto Mara (Mara Day) yatakayofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Maasai Mara,  Jimbo la Narok, Jamhuri ya  Kenya.

Maadhimisho ya siku ya Mara huadhimishwa kila mwaka kwa pamoja kati ya Tanzania na Kenya ambazo ni Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hufanyika kwa pamoja ili kusherehekea mazingira ya Mto Mara na faida zake kwenye maisha yao.

Kwa mwaka huu Maadhimisho haya yamepangwa kufanyika tarehe 15th Septemba, 2014 na yatahudhuriwa na watu mashuhuri kutoka Tanzania na Kenya, wawakilishi kutoka serikali za majimbo ya Narok na Bomet, Mkoa wa Mara, Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria(LVBC), Mashule, Sekta Binafsi na wawakilshi wa  asasi za Kijamii.

Tarehe “15th Septemba  ilikubaliwa na Baraza la Mawaziri la kumi(10) la Kisekta ya Bonde la Ziwa Victoria  Tarehe 4 Mei,2012 Kigali – Rwanda kuwa siku ya Mara yaani  ‘Mara Day’.

Maelekezo ya Baraza yanaongeza chachu kwenye utekelezaji wa sera ya usimamizi endelevu wa Mto Mara na Mazingira yake katika Bonde la Ziwa Victoria” na juhudi za Nchi za Tanzania na Kenya na serikali ya majimbo ya Narok,Bomet na Mkoa wa Mara hazina Budi kupongezwa kwa maandalizi ya siku hii yatakayopelekea kufanikisha maadhimisho haya.

Serikali za Tanzania na Kenya na Wadau wa maendeleo kama vile Shirika la Maendeleo la Kimarekani (USAID), World Wide for Nature (WWN), Nile Equatorial Lakes Subsidiary Action Program (NELSAP) na Sekta binafsi zimekuwa msaada mkubwa katika kuendeleza Mazingira ya Mto Mara.  

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Kenya wameahidi kushirikiana katika usimamizi endelevu wa Bonde la Mto Mara kama mazingira ya kiasili katika bonde la Ziwa Victoria linalochangia katika maendeleo endelevu ya kijamii, utunzaji mazingira na uhai wa uchumi wa nchi hizi. 

LVBC wanachukulia juhudi za ushirikiano wa Nchi hizi Wanachama kama hatua muhimu za kusimamia na kuendeleza rasilimali za jamii zilizozunguka maeneo haya ili kuweza kuchangia katika agenda za mtangamano wa Afrika Mashariki.   

Sekta binafsi na Asasi za Kijamii zinazozunguka jamii hizi sio tu kushiriki katika siku ya Mara bali kushiriki kikamilifu katika usimamizi endelevu wa mto Mara kwa kuwa maisha ya mamilioni ya watu na viumbe mbalimbali vya Hifadhi maarufu duniani ya Serengeti na mbuga ya Maasai Mara yanategemea ustawi wa Mazingira haya.

Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Mara Milele” na maadhimisho haya yanafanyika kipindi hiki muafaka ambacho uhamaji mkubwa wa Nyumbu na Wanyama wengine, ambapo inakadiriwa jumla ya Nyumbu milioni mbili(2) wanahama kutoka mbuga ya Serengeti- Tanzania kwenda mbuga ya Maasai – Mara Kenya kwa kipindi cha Julai mpaka Octoba kila Mwaka. Uhamaji huu ni kati ya Maajabu saba mapya ya Dunia.

Maadhimisho ya tatu(3) ya siku ya Mto Mara  yatatanguliwa na mkutano na vyombo vya habari, kupanda mti, michezo mbalimbali na shughuli nyingine ili kufanikisha maadhimisho haya. Matukio haya yatafanyika kama sehemu ya kuadhimisha Mto Mara kama rasilimali ya kikanda kwa maendeleo endelevu ya Bonde la Ziwa Victoria na kuongeza uelewa kwa wadau kwenye changamoto na umuhimu wa bonde la Mto Mara. 

Maazimisho haya ya Mto Mara yanalenga kujenga uelewa wa ekologia Mto huu kama rasilimali ya pamoja ya kikanda baina ya Nchi hizi mbili kwa kuwezesha wadau wa Mto mara umuhimu wa utunzaji bonde la mto Mara na viumbe vilivyomo kwa maendeleo ya Jamii zinazozunguka maeneo haya na Taifa kwa Ujumla.
    
“Maadhimisho ya Mto Mara yanapelekea mwonekano wa  mali asili zilizoko katika ukanada wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na umuhimu uliopo kwenye maliasili hii kwa maisha ya viumbe na uchumi wa Nchi hizi mbili.


IMETOLEWA NA WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

Thursday, 28 August 2014





Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Margaret Zziwa akizungumza kwenye ufunguzi wa bunge hilo.
3. Spika wa Bunge la Tanzania Anne Makinda (kushoto) akiwa na Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Margaret Zziwa wakati wa ufunguzi wa vikao vya bunge hilo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam 27August, 2014.




Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Margaret Zziwa akizungumza kwenye ufunguzi wa bunge hilo.
3. Spika wa Bunge la Tanzania Anne Makinda (kushoto) akiwa na Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Margaret Zziwa wakati wa ufunguzi wa vikao vya bunge hilo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam 27August, 2014.


Spika wa Bunge la Tanzania Anne Makinda akihutubia Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) la kwanza kufanyika Dar es Salaam, tangu kuanza kwa utaratibu wa kufanyika kwa bunge hilo kwa mzunguko kwa kila nchi mwanachama wa Jumuiya. 

                                                     

Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Dkt. Abdullah Juma Abdullah  Saadalla (wa pili kushoto), akifuatilia ufunguzi wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki.Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki, Phyllis Kandie  (Waziri kutoka Kenya) Shem Bagaine (Waziri kutoka Uganda), Leontine Nzeyimana (Waziri kutoka Burundi), Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Richard Sezibera na kushoto ni Mwanasheria Mkuu wa Jumuiya hiyo  Wilbert Kaahwa.

                                                            



Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika  Mashariki (EALA) wakiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge hilo Dkt. Margaret Zziwa (wa nne kutoka kulia waliokaa) na Spika wa Bunge la Tanzania Anne Makinda, mara baada ya ufunguzi wa bunge hilo.


                                                         

Friday, 15 August 2014

UFUNGUZI NA UZINDUZI WA MAONYESHO YA WAJASILIA MALI NA KIWANDA CHA SMOKE HOUSE STORE LIMITED MJINI BAGAMOYO

Katibu Mkuu wa Wizara ya ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi Joyce Mapunjo akihutubia Wajasilia Mali wadogo mjini Bagamoyo wakati wa Ufunguzi wa Maonesho hayo yaliyoanza tarehe 14/8/2014.


Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kulia) Bi Joyce Mapunjo akitembelea moja ya banda la mjasiliamali katika maonyesho ya wajasilia mali  mjini Bagamoyo mara baada ya kufungua maonesho hayo.
                                                                      

                                                                             
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi Joyce Mapunjo akikata utepe kufungua kiwanda cha  kusindika Mvinyo utokanao na mmea wa Rozera  cha SMOKE HOUSE STORE LIMITED kinacho milikiwa na Bi Teddy Devis kilichopo Mkoa wa Pwani Wilaya ya Bagamoyo. 



Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Ndugu Bi. Joyce Mapunjo akipewa maelekezo na mmoja wa wajasilia mali alipo tembelea banda hilo.