JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
Simu ya maandishi: ‘MEAC’
Simu Na. 022-2126827, 2126830, 2126823
Fax: 022 –
2126651/2120488
Barua Pepe: ps@meac.go.tz
Tovuti: www.meac.go.tz
|
NSSF
Waterfront Ghorofa ya 5
35 Barabara
ya Edward Sokoine
S.L.P 9280,
11467 DAR ES
SALAAM,
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Mkutano wa Sita
wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) kuanza Leo Jijini Arusha,
Tanzania.
Bunge
la Jumuiya ya Afrika Mashariki limeanza Mkutano wake leo Mei 23, 2016 Jijini
Arusha, Tanzania. Mkutano huu wa Sita, Kikao cha Nne wa Bunge la Tatu
unatarajiwa kufanyika kwa siku 12 kuanzia leo Jumatatu Mei, 23 hadi Ijumaa Juni
3, 2016.
Bunge
hili katika Vikao vyake linatarajiwa kuongozwa na Spika wa Bunge hilo, Mhe.
Daniel Kidega. Moja kati ya ajenda kuu katika Bunge hili ni kusomwa kwa Hotuba
ya Bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na
Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt.
Augustine Mahiga Mei 26, 2016. Baada ya bajeti kusomwa watajadili na kupitisha
Bajeti hiyo ikiwa ni moja ya sehemu ya majukumu yaliyopo kwenye Mamlaka yao.
Hotuba
ya Bajeti ni shughuli muhimu katika utekelezaji wa Kalenda ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki. Mwaka wa fedha 2015/2016 EALA ilijadili na kupitisha makadirio ya
Bajeti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Jumla ya Dola za Kimarekani 110,660,098.
Bajeti
ya mwaka 2015/2016 ilitoa kipaumbele katika utekelezaji wa hatua mbili muhimu
za Mtangamano; Himaya ya Umoja wa Forodha na Itifaki ya Soko la Pamoja ambayo
ililenga kuipandisha hadhi Pasi ya kusafiria ya Afrika Mashariki kuwa ya Kimataifa, kuboresha mazingira ya
biashara ndani ya Jumuiya, na kuboresha mfumo wa malipo.
Katika
hatua nyingine EALA katika Mkutano
wake wa wiki mbili linatarajiwa kuhutubiwa na Wake wa Marais Waasisi wa Jumuiya
ambao ni Mama Maria Nyerere (Mke wa Baba wa Taifa na Rais wa awamu ya kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mw. Julius
Kambarage Nyerere), Mama Maria Obote (Mke wa Rais wa zamani wa Uganda Hayati
Milton Obote) na Mama Ngina Kenyatta (Mke wa Rais wa zamani wa Kenya Hayati
Jomo Kenyatta). Katika tukio hili litakalo fanyika Mei 30, 2016 pia itakuwa ni
fursa pekee kwa Wabunge wa EALA na watendaji wengine mbalimbali kubadilishana
uzoefu na Wake wa Marais Wastaafu, ikizingatiwa kuwa Jumuiya ya sasa imechukua
misingi muhimu ya kiutendaji kutoka kwa Jumuiya ya awali.
Katika
Bunge hili la Sita Muswada wa Sheria wa watu wenye ulemavu wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki pia unatarajiwa kujadiliwa.
Aidha,
Bunge linatarajia kupokea na Kujadili ripoti mbalimbali kutoka kwa kamati zake.
Ripoti hizo ni pamoja na;
·
Ripoti
kutoka kamati ya Mawasiliano Biashara na uwekezaji na,
·
Ripoti
kutoka kamati ya malengo ya pamoja,
Vilevile
Bunge litasimamia vikao vya majadiliano ya kamati zake juu ya misuada na
Masuala mbalimbali ya Jumuiya katika kipindi chote cha wiki mbili za Mkutano
wake.