Monday, 19 January 2015

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Bw. Amantius C. Msole akiwa katika Mkutano wa kuwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara kwa Kipindi cha Julai – Desemba, 2014 kwa Kamati ya Bunge kwenye Mkutano uliofanyika katika Ofisi ndogo za Bunge Jijini Dsm
Waziri Mh. Samuel Sitta (kulia) akisikiliza maoni ya mjumbe (hayumo pichani) wakati wa uwasilishwaji wa Taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara kwa kipindi cha Julai – Desemba, 2014 kwa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa 16/1/2015.

Waziri Mh. Samuel Sitta (kulia) akiwa na Naibu Waziri Mh. Dk. Abdulla .J. Saadalla (Kushoto) wakati akisisitiza jambo kwenye Mkutano wa kuwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara kwa kipindi cha Julai - Disemba, 2014 kwa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika Ofisi ndogo za Bunge zilizopo Jijini Dar-es-Salaam Tarehe 16/1/2015

Waziri Mh. Samuel Sitta (kulia) akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara kwa kipindi cha Julai – Desemba, 2014 kwa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Tarehe 16/1/2015.


Thursday, 15 January 2015

Wajumbe kutoka Kenya wakiwa katika picha ya pamoja na Wataalam wa Wizara mara baada ya Mkutano wakujadili Masuala mbalimbali yanayohusu Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa upande wa Tanzania na Kenya uliofanyika Hotel ya Ledger Jijini Dsm Tarehe 14/1/2015.

Saturday, 10 January 2015

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar Bw. Said A.S Natepe akisaini Kitabu cha Wageni alipotembelea Banda la Wizara kwenye Tamasha la Pili la Biashara Zanzibar lililofanyika katika Uwanja wa Maisara Mjini Unguja Tarehe 5- 12/1/2015.

Baadhi ya Wananchi waliotembelea Banda la Wizara kwenye Tamasha la Pili la Biashara Zanzibar wakisaini Kitabu cha Wageni. Tarehe 9/1/2015
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Wizara Bi. Robi Bwiru na Maofisa wengine wa Wizara wakitoa Elimu kwa Wananchi waliotembelea Banda la Wizara kwenye Tamasha la Pili la Bishara Zanzibar Tarehe 9/10/2015. 

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji Dr. Abdullah Makame (Kulia) akiwa kwenye Sherehe za Ufunguzi wa Tamasha la Pili la Bishara Zanzibar Kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara Tarehe 9/1/2015.


Mgeni Rasmi, Makamu wa Pili wa Raisi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  Balozi Seif Ali Idd (kulia) akipewa maelezo na Maofisa wa Wizara (hawapo pichani) alipotembelea Banda la Wizara mara baada ya Sherehe za Ufunguzi wa Tamasha la Pili la Biashara Zanzibar.