Tuesday 22 September 2015

Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mbogo Futakamba (kushoto) na Waziri wa Wizara ya Maji kutoka Nchini Kenya Mhe. Eugine Wamarwa (kulia) wakisaini Mkataba wa Makubaliano ya kuhifadhi Bonde la Mto Mara kwenye Maadhimisho ya Mara Day 15/09/2015, yaliyofanyika katika Uwanja wa Mwenge mjini Butiama. Maonesho haya yanayolenga kuhamasisha uhifadhi wa Bonde la Mto Mara kwa wananchi wa Tanzania na Kenya yameadhimishwa kwa mara ya tatu mwaka huu tangu yaanzishwe mwaka 2012.
Katibu Mkuu Bibi Joyce Mapunjo akizungumza na wananchi (hawapo pichani) waliojitokeza kwenye maadhimisho ya Mara Day yaliyofanyika Butiama katika uwanya wa Mwenge15/09/2015
Katibu Mkuu Bibi Joyce Mapunjo akizungumza na wananchi (hawapo pichani) waliojitokeza kwenye maadhimisho ya Mara Day yaliyofanyika Butiama katika uwanya wa Mwenge15/09/2015.
Wananchi wakiwa wamebeba bango la kuhamasisha utunzaji wa Bonde la Mto Mara siku ya Maadhimisho ya Mara Day yaliyofanyika Wilaya ya Butiama Mkoani Mara 15/09/2015.
Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal (wakwanza kushoto), Katibu Mkuu Bibi Joyce Mapunjo (wakwanza kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Luten Mstaafu Aseri Msangi (katikati) wakiwasalimia wananchi waliojitokeza kwenye maadhimisho ya Mara Day15/09/2015
Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal (kushoto) akikabithiwa machapisho yenye ujumbe mbalimbali kuhusu masuala ya Jumuiya na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Miundombinu ya Kiuchumi na Huduma za Kijamii Bw. Eliabi Chodota (kulia) tar. 15/09/2015

HABARI KATIKA PICHA

Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal (kushoto) akizungumza Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Miundombinu ya Kiuchumi na Huduma za Kijamii Bw. Eliabi Chodota alipotembelea banda la Wizara kwenye maadhimisho ya Siku ya Mara (Mara Day)15/09/2015, yaliyofanyika katika Uwanja wa Mwenge mjini Butiama. Maonesho haya yanayolenga kuhamasisha uhifadhi wa Bonde la Mto Mara kwa wananchi wa Tanzania na Kenya  yameadhimishwa kwa mara ya tatu mwaka huu tangu yaanzishwe mwaka 2012.
Makamu wa Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal akimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Miundombinu ya Kiuchumi na Huduma za Kijamii Bw. Eliabi Chodota alipotembelea banda la Wizara kwenye maadhimisho ya Mara Day yaliyofanyika katika Uwanja wa Mwenge mjini Butiama. Maonesho haya yanayolenga kuhamasisha uhifadhi wa Bonde la Mto Mara kwa wananchi wa Kenya na Tanzania  yameadhimishwa kwa mara ya tatu mwaka huu tangu yaanzishwe mwaka 2012.
Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal (kushoto) akizungumza na Katibu Mkuu Bibi. Joyce Mapunjo (watatu kulia)alipotembelea banda la Wizara kwenye maadhimisho ya Mara Day yaliyofanyika Butihama katika uwanja wa mwenge tah12-15/09/2015
Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mbogo Futakamba (kushoto) na Waziri wa Wizara ya Maji kutoka Nchini Kenya Mhe. Eugine Wamarwa (kulia) wakipeana Mkono wa pongezi mara baada ya kusaini Mkataba wa Makubaliano ya kuhifadhi Bonde la Mto Mara 15/09/2015.
Katibu Mkuu Bibi Joyce Mapunjo (wakwanza kushoto) akiwa kwenye mkutano na wadau wa kuzalisha na kuuza mchele, Mkutano huu ulilenga kuzungumzia utekelezwaji wa Sera ya kuongeza dhamani ya mchele ili kuwawezesha wananchi kunufaika na soko la ndani ya Nchi na la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika itifaki ya Soko la Pamoja.Katika ni Mwenyekiti wa Tanzania Private Sector Foundation Bw. Regnald Mengi. 18/09/2015
Katibu Mkuu Bibi Joyce Mapunjo akizungumza na Wadau kwenye mkutano na wadau wa kuzalisha na kuuza mchele (hawapo pichani) 18/09/2015.
Afisa kutoka Wizarani Bw. Joseph Mbuya (kushoto) akigawa machapisho kwa wananchi waliotembelea banda la Wizara kwenye maadhimisho ya Mara Day yaliyofanyika Mjini Butihama katika uwanja wa Mwenge 15/09/2015.
Wananchi wakipata elimu juu ya masuala mbalimbali ya Jumuiya walipotembelea banda la Wizara wakati wa Maadhimisho ya Mara day yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Mwenge Mjini Butiama

Taswila ya Bango linaloainisha Taratibu za Kufuatwa na Wafanya Biashara wadogo wakati wa Kuuza au Kununua bidhaa ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki lililopo mpaka wa Hororo.