JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA
YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
Simu ya maandishi: ‘MEAC’
Simu Na. 022-2126827, 2126830, 2126823
Fax: 022 –
2126651/2120488
Barua Pepe: ps@meac.go.tz
|
|
NSSF Waterfront Ghorofa ya 5
35 Barabara ya Edward Sokoine S.L.P. 9280,
11467 DAR ES SALAAM.
13/08/ 2015.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
MKUTANO
WA 32 WA BARAZA LA MAWAZIRI
Mkutano
wa 32 wa Baraza la Mawaziri unatarajiwa kufanyika kesho tarehe 14 Agosti,2015 Jijini
Arusha Tanzania. Mkutano huu wa Baraza la Mawaziri unafanyika kesho ukiwa
umetanguliwa na Vikao vya Maafisa Wandamizi wa Serikali na Kamati ya Uratibu
(Makatibu Wakuu) ambavyo vilifanyika kuanzia tarehe10 hadi 13 Agosti, 2015.
Pamoja
na mambo mengine Baraza la Mawaziri litajadili na kuzingatia mambo yafuayo;
- Taarifa ya Tume ya Ukaguz
- Taarifa ya utekelezajia wa mazimio yalifanywa na Mkutano wa Baraza la Mawaziri uliopita
- Taarifa ya Mkutano wa 22 wa Kisekta wa Baraza la Mawaziri wanaosimamia masuala na mipango ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
- Taarifa ya Kikosi kazi cha ngazi ya juu kinacho shughulikia masuala ya marekebisho ya Mkataba wa uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Vilevile
moja ya ajenda itakayo jadiliwa katika Mkutano huu wa 32 wa Baraza la Mawaziri
itahusu Mkutano wa kwanza wa Kilele wa Wafanyabiashara wanaomiliki Viwanda vya
Uzalishaji uanaotarajiwa kufanyika Jijini Kampala, Uganda tarehe 1 hadi 2,
Septemba 2015.
Aidha,
Baraza litajadili na kuzingatia ripoti kutoka taasisi mbalimbali zilizopo chini
ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwemo ripoti ya Taasisi ya Shirikisho la Vyuo
Vikuu vya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki
Imetolewa
na;
Katibu Mkuu
WIZARA YA
USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI