TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Zaidi ya watu 300,000
wanatarajiwa kuhudhuria Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Mto Mara (Mara Day)
yatakayofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Maasai Mara, Jimbo la Narok, Jamhuri ya Kenya.
Maadhimisho ya siku ya
Mara huadhimishwa kila mwaka kwa pamoja kati ya Tanzania na Kenya ambazo ni
Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hufanyika kwa pamoja ili
kusherehekea mazingira ya Mto Mara na faida zake kwenye maisha yao.
Kwa mwaka huu Maadhimisho
haya yamepangwa kufanyika tarehe 15th Septemba, 2014 na yatahudhuriwa na
watu mashuhuri kutoka Tanzania na Kenya, wawakilishi kutoka serikali za majimbo
ya Narok na Bomet, Mkoa wa Mara, Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria(LVBC),
Mashule, Sekta Binafsi na wawakilshi wa
asasi za Kijamii.
Tarehe “15th Septemba ilikubaliwa na Baraza la Mawaziri la kumi(10)
la Kisekta ya Bonde la Ziwa Victoria Tarehe
4 Mei,2012 Kigali – Rwanda kuwa siku ya Mara yaani ‘Mara Day’.
Maelekezo ya Baraza
yanaongeza chachu kwenye utekelezaji wa sera ya usimamizi endelevu wa Mto Mara
na Mazingira yake katika Bonde la Ziwa Victoria” na juhudi za Nchi za Tanzania
na Kenya na serikali ya majimbo ya Narok,Bomet na Mkoa wa Mara hazina Budi
kupongezwa kwa maandalizi ya siku hii yatakayopelekea kufanikisha maadhimisho
haya.
Serikali za Tanzania na
Kenya na Wadau wa maendeleo kama vile Shirika la Maendeleo la Kimarekani (USAID),
World Wide for Nature (WWN), Nile Equatorial Lakes Subsidiary Action Program
(NELSAP) na Sekta binafsi zimekuwa msaada mkubwa katika kuendeleza Mazingira ya
Mto Mara.
Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Jamhuri ya Kenya wameahidi kushirikiana katika usimamizi endelevu
wa Bonde la Mto Mara kama mazingira ya kiasili katika bonde la Ziwa Victoria
linalochangia katika maendeleo endelevu ya kijamii, utunzaji mazingira na uhai
wa uchumi wa nchi hizi.
LVBC wanachukulia juhudi
za ushirikiano wa Nchi hizi Wanachama kama hatua muhimu za kusimamia na kuendeleza
rasilimali za jamii zilizozunguka maeneo haya ili kuweza kuchangia katika
agenda za mtangamano wa Afrika Mashariki.
Sekta binafsi na Asasi za
Kijamii zinazozunguka jamii hizi sio tu kushiriki katika siku ya Mara bali kushiriki
kikamilifu katika usimamizi endelevu wa mto Mara kwa kuwa maisha ya mamilioni
ya watu na viumbe mbalimbali vya Hifadhi maarufu duniani ya Serengeti na mbuga
ya Maasai Mara yanategemea ustawi wa Mazingira haya.
Kauli mbiu ya Maadhimisho
ya mwaka huu ni “Mara Milele” na maadhimisho haya yanafanyika kipindi hiki
muafaka ambacho uhamaji mkubwa wa Nyumbu na Wanyama wengine, ambapo inakadiriwa
jumla ya Nyumbu milioni mbili(2) wanahama kutoka mbuga ya Serengeti- Tanzania
kwenda mbuga ya Maasai – Mara Kenya kwa kipindi cha Julai mpaka Octoba kila
Mwaka. Uhamaji huu ni kati ya Maajabu saba mapya ya Dunia.
Maadhimisho ya tatu(3) ya
siku ya Mto Mara yatatanguliwa na
mkutano na vyombo vya habari, kupanda mti, michezo mbalimbali na shughuli
nyingine ili kufanikisha maadhimisho haya. Matukio haya yatafanyika kama sehemu
ya kuadhimisha Mto Mara kama rasilimali ya kikanda kwa maendeleo endelevu ya
Bonde la Ziwa Victoria na kuongeza uelewa kwa wadau kwenye changamoto na
umuhimu wa bonde la Mto Mara.
Maazimisho haya ya Mto
Mara yanalenga kujenga uelewa wa ekologia Mto huu kama rasilimali ya pamoja ya
kikanda baina ya Nchi hizi mbili kwa kuwezesha wadau wa Mto mara umuhimu wa
utunzaji bonde la mto Mara na viumbe vilivyomo kwa maendeleo ya Jamii zinazozunguka
maeneo haya na Taifa kwa Ujumla.
“Maadhimisho ya Mto Mara
yanapelekea mwonekano wa mali asili
zilizoko katika ukanada wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na umuhimu uliopo kwenye
maliasili hii kwa maisha ya viumbe na uchumi wa Nchi hizi mbili.
IMETOLEWA
NA WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI