Monday, 6 July 2015

HABARI KATIKA PICHA JUU YA MATUKIO MBALIMBALI YALIYOJILI KWENYE MAONESHO YA SABASABA NA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

Mkurugenzi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji Bw. Geoffrey Mwambe (mwenye fulana nyeupe)akizungumza na wajasiriamali toka Kenya alipotembelea banda lao kwenye maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba Jijini Dar 04/07/2015.
Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili Mhe. Alhaj Ali Hassan Mwinyi (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Bw. Amantius C. Msole wakifurahia jambo siku ya kilele cha wiki ya utumishi wa Umma katika viwanja vya Mnazi mmoja Dsm 23/06/02015.
 Watumishi Wizara wakiwa katika Picha ya Pamoja kwenye banda la Wizara tayari kwa kutoa elimu kwa umma juu ya masuala mbalimbali ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika Viwanja vya Mnazi mmoja Dar es Salaam.
Mwananchi akiomba ufafanuzi wa jambo kutoka kwa Maafisa wa Wizara kwenye maadhimisho ya Wiki ya Utumishi  wa Umma iliyo adhimishwa katika Viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam.
Afisa wa Wizara Bw. Amedeus Mzee (wapili kushoto) akifafanua jambo kwa mwananchi aliyetembelea banda la Wizara kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma katika Viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji Bw. Godffrey Mwambe (kulia) akifafanua kwa mwandishi wa habari aliyetembelea banda la Wizara kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma katika Viwanja vya Mnazimmoja Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Miundombinu ya Kiuchumi na Huduma za Kijamii Bw. Eliabi Chodota (katikati) akifafanua jambo kwa mwandishi wa habari aliyetembelea banda la Wizara kwenye Wiki ya Maadhimisho ya Utumishi wa Umma iliyoadhimishwa kwenye Viwanja vya Mnazimmoja Jijini Dar es Salaam
Mhe. Balozi Chiravi Ali Mwakwere anayeiwakilisha Kenya Nchini Tanzania akisaini Kitabu cha wageni alipotembelea banda la Wizara katika maonesho ya Kimataifa ya 39 ya Biashara Sabasaba alipotembelea banda hilo Jijini Dar es Salaam 01/07/2015.
Mkurugenzi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji Bw. Geoffrey Mwambe (katika) akiangalia bidhaa za mfanyabiashara toka Burundi alipotembelea banda la Mjasiriamali huyo kwenye maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba Dsm 04/07/2015.
Mkurugenzi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji Bw. Geoffrey Mwambe (kushoto) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Baraza la Kukuza Mauzo ya Nje la Kenya (Export Promotion Council) kwenye maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba Dsm 04/07/2015. Kulia ni Meneja wa Taarifa za Biashara na Huduma wa Baraza hilo
Bw. Charles Tumbo 04/07/2015.

Wananchi wakiwa wamekusanyika kwa wingi kwenye banda la Wizara lililopo kwenye Maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba ili kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kutoka kwa maafisa wa Wizara 06/07/2015

Wananchi wakiwa wamekusanyika kwa wingi kwenye banda la Wizara lililopo kwenye Maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba ili kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kutoka kwa maafisa wa Wizara 06/07/2015
Naibu katibu Mkuu Bw. Amantius C. Msole akiwa kwenye banda la Wizara katika Maonesho ya Kimataifa ya 39 ya Biashara Sabasaba alipo tembelea banda hilo Jijini Dar es Salaam 01/07/2015.

No comments:

Post a Comment