Monday, 6 July 2015

Wananchi wakiwa wamekusanyika kwenye Banda la Wizara kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kutoka kwa Maafisa wa Wizara waliopo katika banda la Wizara kwenye Maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa  Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam 06/07/2015.
Wananchi wakiwa wamekusanyika kwenye Banda la Wizara kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kutoka kwa Maafisa wa Wizara waliopo katika banda la Wizara kwenye Maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa  Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam 06/07/2015.
Mkurugenzi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji Bw. Geoffrey Mwambe (kushoto) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Banda la Kenya  la Baraza la kukuza Mauzo ya Nje (Export Promotion Council) lililopo kwenye Maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba Jijini Dar es Salaam, Kulia ni Meneja wa Baraza hilo Bw. Charles Tumbo 4/07/2015.
Mkurugenzi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji Bw. Geoffrey Mwambe (aliyevalia fulana nyeupe) akizungumza na Wafanyabiashara toka Kenya waliokuja kushiriki katika Maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam 04/07/2015
Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili Mhe. Alhaj Ali Hassan Mwinyi (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Bw. Amentius Msole wakifurahia jambo siku ya kilele cha Wiki ya Utumishi wa Umma katika viwanja vya Mnazimmoja Dar es Salaam23/06/02015. Mhe. Rais Mstaafu alikuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho hayo.
Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili Mhe. Alhaj Ali Hassan Mwinyi (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Bw. Amentius Msole wakiwa tayari  kutoa tuzo kwa washiriki walioshinda tuzo mbalimbali katika maadhimisho ya Kilele cha Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazimmoja Jijini Dar es Salaam 23/06/2015.
Naibu Katibu Mkuu alipotembelea banda la Wizara siku ya ufunguzi wa Maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam 03/07/2015.
Mhe. Balozi Chiravi Ali Mwakwere anayeiwakilisha Kenya Nchini Tanzania akisaini Kitabu cha wageni alipotembelea banda la Wizara katika Maonesho ya 39 ya Biashara  ya Kimataifa Sabasaba Jijini Dar es Salaam 01/07/2015.
Mkurugenzi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji Bw. Godffrey Mwambe (katika) akiangalia bidhaa za mfanyabiashara toka Burundi alipotembelea banda lake kwenye Maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam 04/07/2015.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu ya Kiuchumi na Huduma za Kijamii Bw. Eliabi Chodota (katikati) akifafanua jambo kwa mwandishi wa habari alipotembelea banda la Wizara kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazimmoja Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji Bw. Geoffrey Mwambe (kulia) akifafanua jambo kwa mwandishi wa habari aliyetembelea banda la Wizara kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazimmoja Jijini Dar es Salaam.
Watumishi wa Wizara wakimsikiliza mwananchi aliyetembelea banda la Wizara kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazimmoja Jijini Dar es Salaam.
Watumishi wa Wizara wakiwa katika Picha ya pamoja kwenye banda la Wizara katika Wiki ya Maadhimisho ya Utumishi wa Umma tayari kwa kutoa elimu kwa Umma  juu ya Masuala mbalimbali ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Maadhimisho hayo yalifanyika katika Viwanja vya Mnazimmoja Jijini Dar es Salaam 
Watumishi wa Wizara wakimsikiliza mwananchi aliyetembelea banda la Wizara kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazimmoja Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bibi. Robi E. Bwiru akifafanua jambo kwa mwananchi aliyetembelea banda la Wizara kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazimmoja Jijini Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment