Thursday, 30 April 2015

Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu ya Kiuchumi na Huduma za Kijamii Bw. George P.E. Lauwo (Kulia) akikabidhiwa Mkasi na Mkurugenzi Mkazi wa TradeMark East Afrika  Bw. Josaphat Kweka (kushoto) wakati wa uzinduzi wa ripoti ya utekelezaji wa Miradi ya shirika hilo kwa mwaka 2013/2014 katika Hoteli ya Serena Dar-es-Salaam. TradeMark East Afrika (TMEA) ni Shirika lisilo la Kiserikali linalofadhili Miradi mbalimbali ya Kibiashara Afrika Mashariki ikiwemo Mradi wa Ujenzi wa Vituo vya Utoaji Huduma Pamoja Mpakani.

Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu ya Kiuchumi na Huduma za Kijamii Bw. George P.E. Lauwo (kulia) akikata utepe wakati akizindua ripoti ya utekelezaji wa Miradi ya Shirika la TradeMark East Afrika katika Hoteli ya Serena Dsm, Kushoto ni Bw. Josaphat Kweka Mkurugenzi Mkazi wa Shirika hilo 30/4/2015.

Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu ya Kiuchumi na Huduma za Kijamii Bw. George P.E. Lauwo akionesha ripoti ya utekelezaji wa Miradi ya TradeMark East Afrika 2013/2014 mara baada ya uzinduzi wa ripoti hiyo uliofanyika katika Hoteli ya Serena Dsm 30/4/2015.


No comments:

Post a Comment