Wednesday, 21 October 2015

HABARI KUHUSU TIMU YA WAANGALIZI WA UCHAGUZI OCTOBA 25, 2015 YA EAC

     Katibu Mkuu Bibi Joyce Mapunjo (wa kwanza kushoto kati ya waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na timu ya waangalizia wa uchaguzi Nchini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki mara baada ya mkutano na wanahabari uliofanyika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar 20/10/2015.
      Kiongozi wa timu ya uangalizi wa uchaguzi nchini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambaye pia ni Makamu wa Rais wa zamani wa Kenya Mhe. Dkt. A. A Moody Awori akiongea kwenye mkutano na wanahabari uliofanyika katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar 20/10/2015
     Katibu Mkuu Bibi Joyce Mapunjo akiongea kwenye Mkutano na wanahabari (hawako pichani) uliondaliwa na Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar 20/10/2015
    Mmoja wa waangalizi wa Uchaguzi Nchini kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Charles Njoroge akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kwenye mkutano uliofanyika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es Salaam 20/10/2015.  
      Naibu Katibu Mkuu Bw. Amantius C. Msole (kulia), Mkurugenzi Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama Bw. Stephen Mbundi (katikati) na mmoja wa waangalizi wa uchaguzi kutoka SADC (kushoto) wakiwa kwenye Mkutano na wanahabari uliondaliwa na Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es Salaam 20 Oktoba, 2015.
Katibu Mkuu Bibi Joyce Mapunjo (katikati) akiwa kwenye mkutano na wanahabari ulioandaliwa na Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kushoto ni Mbunge wa EALA Mhe. Peter Muthuki, na Makamu wa Rais wa zamani wa Kenya Mhe. Dkt. A. A Moody Awori (kulia) ambaye pia ni Kiongozi wa timu ya waangalizi wa uchaguzi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
WAANGALIZI WA UCHAGUZI KUTOKA EAC WAHIMIZWA KUZINGATIA SHERIA NA TARATIBU NCHINI.

Kuelekea uchaguzi Mkuu Nchini unaotarajiwa kufanyika tarehe 25 Oktoba, 2015 Jumuiya ya Afrika Mashariki imeleta timu ya waangalizi yenye jumla ya watu 55 inayohusisha wataalamu na viongozi mbalimbali wa kitaifa wakiwemo wastaafu na wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka nchi wanachama. Timu hii iliwasili Jijini Dar es Salaam 18 Oktoba, 2015. 

Katibu Mkuu Bibi Joyce Mapunjo akizungumza kwenye Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jana katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es Salaam ambao pia ulihudhuriwa na waangalizi kutoka EAC na SADC amewahimiza waangalizi wa uchaguzi kuzingatia sheria na taratibu za Nchi katika shughuli zao. 

Akizungumza katika mkutano huo alisisitiza kuwa Tanzania ni Nchi ya Kidemokrasia na inautaratibu mzuri wa kuachiana madaraka ambapo uchaguzi hufanyika kila baada ya miaka mitano na kubadilsha uongozi wa juu kila baada ya miaka kumi kwa mujibu wa katiba. 

Kiongozi wa timu ya Uchunguzi kutoka EAC ambaye pia ni Makamu wa Rais wa zamani wa Kenya Mhe. Dkt. A. A Mood Awori akizungumza katika Mkutano huo aliipongeza Tanzania kwa kudumisha Demokrasia na Utawala wa kisheria na kuongeza kuwa katika uchaguzi huu Tanzania iendeleze utamaduni wa kudumisha Demokrasia, Utawala Bora na uwajibikaji ili iendelee kuwa na amani na utulivu. 

Timu ya waangalizi ya EAC ambayo itafanya kazi katika vipindi vitatu vinavyotajwa kuwa, Kabla ya uchaguzi, wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi itaangalia mambo yafuatayo; 

· Ushirikishwaji wa vyombo vya habari katika kuripoti masuala        mbalimbali ya uchaguzi 

· Muda wa kutosha wa kampeni 

· Uhuru wa kuendesha shughuli za kisiasa pasipo fujo au vitisho 

· Utolewaji wa elimu ya uraia na upigaji kura 

· Upigaji kura kwa siri, na 

· Ubora wa vifaa vya uchaguzi 

Aidha timu hiyo ya waangalizi itafanya kazi yake Tanzania bara na Visiwani wakati wote wa uwepo wake katika kipindi chote cha uchaguzi. No comments:

Post a Comment