Wednesday, 14 October 2015

MUSWADA WA SHERIA YA MIAMALA YA KIELEKTONIKI WA MWAKA 2014 WAPITISHWAMUSWADA WA SHERIA YA MIAMALA YA KIELEKTONIKI WA MWAKA 2014 WAPITISHWA

Muswada wa Sheria ya Miamala ya Kielektoniki wa Jumuiya ya Afrika mashariki uliokuwa ukijadiliwa na Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (BJAM) katika vikao vyake vinavyoendelea Jijini Nairobi Kenya, Oktoba 9, 2015 lilipitisha muswada wa sheria ya miamala wa kielektoniki wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwa ni moja ya mikakati ya Jumuiya ya kutengeneza mazingira mazuri ya kufanya miamala ya biashara kwa mfumo wa digitali.

Moja ya sababu za msingi zilizokuwa zikitolewa na Wabunge wengi wakati wakichangia mjadala wa kupitishwa kwa Muswada wa sheria hiyo walisema Sheria hii itakuwa ni chachu ya ukuaji uchumi wa Nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki, kwa kuwa inalenga kukuza teknolojia ambayo itatumika kuendesha miamala ya kibiashara ya kieletoniki katika mazingira ya kisasa sambamba na kuboresha ufanisi na usalama kwa watumiaji wa huduma hiyo, pia itakidhi mahitaji ya sasa ya miamala ya kielectoniki katika biashara.

Mjadala juu ya muswada wa sheria hii uliahirishwa katika Mkutano wa kwanza wa Kikao cha Nne cha Bunge la tatu uliofanyika Agosti , 2015 Jijini Kampala, Uganda baada ya Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri Mhe. Dkt. Abdullah Saadala kulieleza Bunge hilo kuwa Muswada huo unahitaji kuboreshwa zaidi na wadau kabla haujapitishwa.

Baada ya kupitishwa kwa Muswada wa sheria hiyo Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki ambaye pia ni Naibu Waziri Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Abdallah Saadala alisema Wabunge walijadili Muswada huo wakiwa na sura moja wakizingatia faida ambazo Nchi wanachama zitanufaika nazo kutokana na sheria hiyo.

No comments:

Post a Comment