Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bw. James Lugaganya (wakwanza kushoto) akiwa na wataalam waelekezi kutoka SAGCOT katika Mkutano uliofanyika jengo la Waterfront Jijini Dar |
Monday, 28 March 2016
WATALAM WAELEKEKEZI KUTOKA SAGCOT WAKUTANA NA WATAALAM WA WIZARA
Friday, 18 March 2016
BUNGE LA EALA KUWAENZI WAKE WA WAASISI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI
Bunge
la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) limepitisha kwa sauti moja hoja ya
kuwaenzi wake wa Marais Waasisi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyopita
(1967-77), wake hao ni Mama Maria Nyerere (Tanzania), Mama Ngina Kenyata(Kenya)
na Mama Mirium Obote (Uganda).
Hoja hii iliwasilishwa Bungeni na Mhe. Mumbi
Ng’aru kutoka Kenya, hoja hii wakati ikiwaslishwa ilivuta hisia za wabunge
wengi, akiongea wakati anawasilisha hoja hiyo aliomba Bunge kuunga mkono hoja
hiyo na kuwaalika katika kikao cha Bunge kinachotarajiwa kufanyika Mei, 2016
Jijini Arusha.
Akiongea
wakati anawailisha hoja hiyo alisema wakati umefika sasa Bunge kutambua mchango
wa wakina mama hawa wanaobeba historia kubwa ya Jumuiya, kwani wakati Marais
hawa wanahangaika na harakati za kuunganisha nchi za Afrika Mashariki wao
walikuwa bega kwa bega na Marais hawa kuwasaidia hasa katika kuwashauri
vizuri na kuaangalia familia, huu ni ukweli usioweza kufumbiwa macho, kwani
akina mama hawa wameendelea kutoa mchango wao kwa Mataifa yetu na Jumuiya yetu
ya sasa kwa kutoa viongozi ambao wanaitumikia Nchi zetu na Jumuiya yetu kwa
namna moja au nyingine.
“Nilibahatika
kuzungumza na akina mama hawa kwa nyakati tofauti, na kwa kweli akina mama hawa
ni zaidi ya maktaba ya masuala ya Afrika Mashariki, ni hadhina ambayo tuna kila
sababu ya kujivunia” alisema Mhe. Mumbi. Wabunge kwa sauti moja walikubaliana
akina mama hawa kualikwa katika Kikao cha Bunge kitakachofanyika Arusha na kuhutubia Bunge hilo.
Wabunge
wengine waliochangia hoja hii kutoka Tanzania ni Mhe. Shyrose Bhanji, Mhe. Makongoro
Nyerere na Mhe. Nderakindo Kessy.
Katika
hatua nyingine Bunge limepitisha ripoti ya Kamati ya Masuala ya Sheria, ripoti
hiyo iliyohusu uoanishaji na uhuishaji wa Sheria za ndani ya Nchi wanachama na
zile za Jumuiya, akichangia wakati wa majadiliano kuhusu ripoti hii Mhe.
Abdullah Mwinyi alisema utekelezaji wa hatua mbalimbali za Mtangamano wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki hasa umoja wa forodha na Soko la Pamoja utategemea
zaidi kuhuishwa kwa sheria hizi kwani sheria nyingi za Nchi wanachama
zinakinzana na zile za Jumuiya hivyo kufanya utekelezaji kuwa mgumu na
wanaoathirika zaidi ni wananchi ambao ndio watumiaji wa sheria hizo.
Bunge hili lilianza vikao vyake tarehe 7 Machi,2016 na kukamilisha Vikao vyake Jana tarehe 17 Machi, 2016, pamoja na mambo mengine Musuada
wa kuzuia usafirishaji haramu wa binadamu (EAC Counter Trafficking in Persons
Bill,2016), ulisomwa kwa mara ya kwanza.
Wednesday, 9 March 2016
WAZIRI MKUU MHE. KASSIM MAJALIWA AHUTUBIA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI (EALA)
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (watatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Waheshiwa Wabunge. |
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Mjaliwa akijadili jambo na Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhe. Daniel Kidega mara baada ya kuahirishwa kwa Mkutano wa Bunge hilo. |
Waheshimiwa Wabunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiendelea Mkutano. |
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akihutubia Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Machi 8, 2016. |
Waziri Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akila kiapo kwa mujibu wa sheria ili awezekushiriki katika Mkutano wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Machi 8, 2016 |
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Mjaliwa akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa 5 wa Bunge la 3 la Afrika Mashariki katika ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania Jijini Dar Machi 8, 2016 |
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akimsiliza Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Daniel Kidega Machi |
Sunday, 6 March 2016
AFRIKA MASHARIKI YAZINDUA EAST AFRICAN COMMUNITY APP
HABARI PICHA; MAKAMU WA RAIS AFUNGUA SEMINA YA 9 YA WABUNGE WA EALA NA WABUNGE WA NCHI WANACHAMA
Friday, 4 March 2016
HABARI PICHA; UZINDUZI WA BARABARA YA ARUSHA-HOLILI-TAVETA-VOI
Baadhi ya Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya vifaa vitakavyo tumika katika ujenzi wa barabara ya Arusha-Holili-Taveta-Voi Machi3, 2016 |
Baadhi ya Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakionesha furaha mara baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa Barabara ya Arusha-Holili-Taveta-Voi Jijini Arusha Machi 23, 2016 |
Tanzania Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa mara nyingine
Tanzania Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa mara nyingine
Katika Hoteli ya Ngurugoto Jijini Arusha Mkutano wa 17 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki chini ya
Mwenyekiti Mhe. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tanzania imeombwa na wakuu wa Nchi hizo kuendelea kushikilia kiti hicho kwa Mwaka mwingine.
Mhe. Rais John Pombe Magufuli akisisitiza jambo |
Mkutano huo ambao ulikuwa wa kipekee kutokana na jinsi Mwenyekiti alivyoeendesha Mkutano, umejadili na kupitisha maamuzi mbalimbali, kati ya maamuzi hayo ni pamoja na kuchagua Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mkutano huu kutokana na matakwa ya Mkataba wa Jumuiya unaoelekeza kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya atakaa na cheo hicho kwa kipindi cha Miaka mitano(5).
Hivyo mkutano huu umemteua Bw. Liberat Mfumukeko kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, madaraka hayo ataanza rasmi kuyatumikia tarehe 26 Aprili,2016 tarehe ambayo Katibu Mkuu wa sasa Dkt. Richard Sezibera atakuwa amemaliza kipindi chake.
Mkutano huu vilevile uliridhia maombi ya kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Jamhuri ya Sudan Kusini, kuridhia kwa maombi haya kunafanya Jumuiya sasa kuwa na Nchi wanachama sita(6). Wakiongea kwa nyakati tofauti Wakuu hawa wa Nchi waliipongeza Nchi ya Sudan ya Kusini na kuwakaribisha katika Jumuiya. “Kila Nchi ina matatizo yake cha muhimu ni kuvumiliana na kuheshimiana ili tuweze kufikia lengo letu la kuwaletea Wanaafrika Mashariki maeendeleo, tunawakaribisha sana wenzetu kutoka Jamhuri ya Sudan, kujiunga kwa Sudan ya Kusini kunafanya Jumuiya kuwa na soko la watu zaidi ya Millioni 150” alisema Mwenyekiti.
Vilevile Mkutano huu umemteua Rais Msataafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Benjamini Wiliam Mkapa kuwa mwezeshaji wa mazungumzo ya kuleta amani Nchi ya Burundi.
Katika Mkutano huu Mwanafunzi Mtanzania Simon S. Mollel kutoka shule ya Sekondari ya Mzumbe alitunikiwa cheti na pesa taslimu kiasi cha Dola za Kimarekani 1500 kwa kuwa mshindi wa kwanza wa shindano la Insha la Jumuiya ya Afrika Mashariki, ushindi wa pili ulichukuliwa na mwanafunzi kutoka Kenya, wa tatu kutoka Rwanda, wanne kutoka Uganda na wa tano kutoka Burundi wote hawa walitunikiwa vyeti na pesa taslimu.
Wakuu wa Nchi katika mkutano huu walizindua Pasi mpya ya kusafiria ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Pasi hii itakuwa ya kisasa kabisa na itaweza kutumika duniani kote, hivyo Wanaafrika Mashariki hawatalazimika kuwa na pasi nyingine, pasi hii inatarajiwa kuanza kutumika rasmi tarehe 1 Januari,2017.
Akiongea katika hotuba ya kufunga mkutano huu wa 17 wa Wakuu wa Nchi, Mwenyekiti wa Wakuu wa Nchi Mhe. John P. Magufuli, aliwasihi watendaji wa Secretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuzingatia matumizi mazuri ya pesa, aliwakumbusha kuwa hizi ni pesa za walipa kodi wa Afrika Mashariki hivyo ni vyema wakazingatia matumizi mazuri ya pesa, alitoa mfano wa matumizi ya ukumbi wa Hoteli ya Ngurudoto ambao ni ghali badala yake Mkutano huu ungeweza kufanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa ‘AICC’ ambao ni bei rahisi na ni Mkubwa.
Akimalizia alisema “ tunatakiwa kuhakikisha kila mwanaafrika mashariki ananufaika na fursa za Jumuiya ya Afrika Mashariki, tusiwe Jumuiya ya kuwanyonya wananchi, yeyote ambaye ataenda kinyume na kuzingatia utaratibu huo sitasita kumripoti kwa Wakuu wa Nchi wenzangu ili atumbuliwe”.
Wakiongea kwa nyakati tofauti wakuu wa Nchi walimpongeza sana Mhe. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyeti wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa jinsi alivyoeendesha Mkutano huu kwa ustadi.
HABARI PICHA; MKUTANO WA 17 WA KAWAIDA WA WAKUU WA NCHI WANACHAMA ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI
Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Kawaida wakifuatilia maendeleo ya Mkutano huo uliofanyika hivi karibuni jijini Arusha |
Viongozi Wakuu wa Nchi Wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakionesha mfano wa pasi za kusafiria ya Afrika Mashariki iliyozinduliwa Machi 2, 2016 Jijini Arusha. |
Mshindi wa Insha Simon S. Mollel kutoka shule ya Sekondari Mzumbe akionesha pesa aliyopewa kama zawadi ya kuwa mshindi wa Kwanza Afrika Mashariki. |
Mhe. Waziri Balozi Dkt. Augustine Mahiga (wakwanza kushoto) akimpongeza Katibu Mkuu mpya wa Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki mara baada ya kuapa. |
Katibu Mkuu mpya wa Sekretariti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Liberat Mfumukeko akiapa mara baada ya kuteuliwa kushisha nafasi hiyo. |
Wajumbe wa mkutano kutoka Tanzania wakifuatilia Mkutano wa 17 Wakawaida wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Jijini Arusha Machi 2, 2016. |
Wajumbe wa Mkutano kutoka Tanzania wakifuatilia Mkutano wa 17 Wakawaida wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Jijini Arusha Machi 2, 2016 |
Wednesday, 2 March 2016
WAZIRI AONGOZA MKUTANO WA 33 WA BARAZA LA MAWAZIRI LA AFRIKA MASHARIKI JIJINI ARUSHA
Mhe. Waziri Balozi Dkt. Mahiga ambaye ni mwenyekiti wa Barala la Mawaziri wa Afrika Mashariki akipokea ripoti ya Kamati ya Ukaguzi na Vihatarishi ya Mwaka 2014/15. |
Baadhi ya Maafisa wa Tanzania wakifuatilia Mkutano |
Mawaziri kutoka Tanzania (walioketi msatari wa mbele) wakifuatilia majadiliano yaliyokuwa yakiendelea katika Mkutano wa 33 wa Baraza la Mawaziri Jijini Arusha tarehe 29 Februari, 2016 |
Subscribe to:
Posts (Atom)