Sunday, 6 March 2016

HABARI PICHA; MAKAMU WA RAIS AFUNGUA SEMINA YA 9 YA WABUNGE WA EALA NA WABUNGE WA NCHI WANACHAMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluh Hassan (wakwanza kulia) akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Semina ya 9 ya kuimarisha uhusiano (Nanyuki 9) kati ya Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki na Wabunge kutoka Nchi Wanachama. Semina hii hufanyika kila mwaka kwa mzunguko katika Nchi Wanachama na kwa mara ya kwanza ilifanyika Nanyuki Nchini Kenya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (watatu kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Waheshimiwa Wabunge na watendaji wa Taasisi zingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki mara baaada ya ufunguzi wa semina ya 9 ya kuimarisha uhusiano (Nanyuki 9) kati ya Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki na Wabunge kutoka Nchi Wanachama.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluh Hassan akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Semina ya 9 ya kuimarisha uhusiano (Nanyuki 9) kati ya Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki na Wabunge kutoka Nchi Wanachama.
Naibu Waziri Mhe. Dkt. Susan Kolimba akihutubia Waheshimiwa Wabunge kwenye Semina ya 9 ya kuimarisha uhusiano (Nanyuki 9) kati ya Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki na Wabunge kutoka Nchi Wanachama.
Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhe. Daniel Kidega akihutubia Wabunge katika Semina ya 9 ya kuimarisha uhusiano (Nanyuki 9) kati ya Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki na Wabunge kutoka Nchi Wanachama iliyofanyika ukumbi wa LAPF Towers Jijini Dar es Salaam Mchi 3, 2016.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akihutubia Waheshimiwa Wabunge kwenye Semina ya 9 ya kuimarisha uhusiano (Nanyuki 9) kati ya Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki na Wabunge kutoka Nchi Wanachama iliyofanyika jijini Dar es Salaam
Baadhi ya waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya ufunguzi wa Semina ya 9 ya kuimarisha uhusiano (Nanyuki 9) kati ya Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki na Wabunge kutoka Nchi Wanachama. Semina hii hufanyika kila mwaka kwa mzunguko katika Nchi Wanachama na kwa mara ya kwanza ilifanyika Nanyuki Nchini Kenya.
No comments:

Post a Comment