Wednesday, 9 March 2016

WAZIRI MKUU MHE. KASSIM MAJALIWA AHUTUBIA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI (EALA)

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (wakwanza kushoto) akiwasili katika ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania ambapo alitoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa 5 wa Bunge la 3 la Jumuiya ya Afrika Mashariki unaoendelea Jijini Dar. Alioambatana nao ni Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhe. Job Ndugai, (aliyetangulia mbele) Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhe. Daniel Kidega (katikati) na Katibu Mkuu wa Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Dkt. Richard Sezibera. Mkutano huu uatafanyika kwa siku 12 kuanzia Machi 6-18, 2016
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (watatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Waheshiwa Wabunge. 
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Mjaliwa akijadili jambo na Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhe. Daniel Kidega mara baada ya kuahirishwa kwa Mkutano wa Bunge hilo.
Waheshimiwa Wabunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiendelea Mkutano.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akihutubia Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Machi 8, 2016.
Waziri Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) akifuatilia Mkutano wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mhe. Balozi Dkt. Mahiga pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Waziri Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akila kiapo kwa mujibu wa sheria ili awezekushiriki katika Mkutano wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Machi 8, 2016
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Mjaliwa akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa 5 wa Bunge la 3 la Afrika Mashariki katika ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania Jijini Dar Machi 8, 2016
Tokea kushoto; Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhe. Daniel Kidega na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai wakishiriki kuimba na kutoa heshima wakati wimbo wa Taifa ukiibwa.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akimsiliza Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Daniel Kidega Machi 
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha wageni kabla ya kutoa hotuba ya ufunguzi wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki linaloendelea na Mkutano wake Jijini Dar, kulia ni Spika wa Bunge hilo Mhe. Daniel Kidega.

No comments:

Post a Comment